Na Esther Clavery,TimesMajira Online TUDARCo
ZAIDI ya wajasiriamali 7,000 wamefikiwa na kupatiwa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yanayotolewa na Taasisi ya Openmind Tanzania katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa mafunzo ya biashara kwa njia ya mtandao (digital marketing) Genoveva Mtiti kutoka taasisi hiyo, wakati akizungumza na wajasiriamali kwenye warsha iliyofanyika Ofisi za Jane Goodall Institute mikocheni.
Amesema taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa wajasiriamali hususani vijana lengo likiwa ni kuwakwamua katika lindi la umasikini kwa kuanzisha miradi mbalimbali.
“Tumeamua kutambua vijana na kuwapa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali hasa haya ya biashara mtandaoni ili waweze kufanya biashara zao kisasa zaidi kwa kutumia mitandao ya kijamii na kupanua wigo wa masoko,” amesema Mtiti.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango