July 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji

Na Israel Mwaisaka,Timesmajiraonline,Nkasi

MAHAKAMA ya Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa imemhukumu kifungo Cha maisha jela Kelvin Pungama (23) mkazi wa Kijiji Cha Karundi Kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka Minne wa darasa la awali katika shule ya msingi Fyengerezya.

Akitoa hukumu hiyo leo hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Nkasi Adamu Mwanjokolo amesema anamtia hatiani mtuhumiwa chini ya kifungu Cha sheria (130) na (2) (e) na 131 (1) na (3) Cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022 ni baada ya mahakama kuridhishwa na maelezo na ushahidi uliotolewa upande wa jamuhuri pasipo kuacha shaka yoyote

Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na waendesha mashtaka wa serikali Irene Mwabeza na Cedric Mashauri waliieleza Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 5,2023 katika Kijiji Cha Nkundi ambapo mtoto huyo alikwenda kumsalimia Dada yake na wakati wakiwa shambani alimuacha mtoto huyo nyumbani na ndipo kijana huyo alipomshika na kumpeleka chumbani kwake na kuanza kumbaka.

Waendesha mashitaka waliiomba Mahakama itoe adhabu Kali Kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho Kwa wengine licha ya kuwa kosa hilo ni kwanza kwake.

Mtuhumiwa Kwa upande wake alikiri kutenda kosa hilo mbele ya Mahakama na kuwa alitenda kosa hilo bila ya yeye kujielewa na kudai kuwa shetani ndiye aliyemfanya atende kosa hilo na ndiyo maana kwa sasa ameokoka na kuiomba Mahakama impunguzie adhabu.

Licha ya utetezi huo Hakimu Mwanjokolo alitoa adhabu ya kifungo Cha maisha jela kwani kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa hakikubaliki katika jamii na amemuathiri mtoto huyo kwa kiasi kikubwa

Wakato huo huo Pia Mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha maisha Cleophas Sumangwa (45) mkazi wa Kijiji Cha Katongolo wilayani Nkasi Kwa kosa la kumbaka Mtoto wa miaka (9) ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Katongolo baada ya kupata maelekezo Kwa Mganga wa kienyeji ili aweze kupata utajiri.

Mtuhumiwa huyo aliweza kumbaka Mtoto huyo mara tatu Kwa siku tofauti na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo Huku akimtisha kwamba asimwambie mtu yeyote juu ya hilo Kwani angeweza kumuua na alikua akimtisha Kwa kisu.

Maelezo ya ushahidi yanaonyesha kuwa mtuhumiwa alikua akimbaka mtoto huyo kwenye shamba la mahindi chini ya mgomba Kila alipokuwa akitoa shule.

Lakini licha ya ushahidi kutolewa mtuhumiwa naye alikiri kutenda kosa hilo na kuwa alidanganywa na Mganga wa kienyeji ili aweze kupata utajiri
hivyo Mahakama ilimkuta na hata mtuhumiwa chini ya kifungu Cha sheria Cha a (130) na (2) (e) na 131 (1) na (3) Cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022 na kufungwa jela kifungo Cha maisha.

Mahakama imesema Kwa yeyote ambaye atakua hajaridhishwa na hukumu hiyo anaweza kukata rufaa mahakama ya juu.