Na David John, TimesMajira online
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewataka wahitimu wa mafunzo kutoka Taasisi ya Uongozi hapa nchini kwenda kuyatumia Mafunzo waliyoyapata vizuri ili kuleta chachu ya mafanikio katika sehemu zao za kazi.
Amesema kuwa ni matumaini yake mafunzo waliyoyapata wanakwenda kuimarisha dhana zima ya Uongozi kwenye sehemu zao za kazi na kuongeza uweledi katika kuchapa kazi.
Ndalichako ameyasema hayo wakati wa mahafari ya nne ya Taasisi ya Uongozi kwa ngazi mbalimbali Kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi ambapo jumla ya wanafunzi 110 walihitimu.
“Imani yangu ni kwamba mmeiva na mmepikwa vizuri zaidi na mtatumia uwezo mliojengewa kuleta mabadiliko chanya kwenye nafasi zenu mnazofanyia kazi na mnaonekana wote mnadhamira kweli ya kuleta matokeo chanya,” amesema Ndalichako
Nakuongeza kuwa “Mkayasimamie maeneo yenu ili kuleta mabadiliko chanya na kimsingi kabla ya kufanya Mafunzo mlifanya tathimini ili kuona maeneo ambayo wanataka kujengewa uwezo zaidi,”amesisitiza Profesa Ndalichako.
Amefafanua kuwa matumaini yake wahitimu hao wanakwenda kuwa mfano zaidi na kwenda kuwa washauri wazuri zaidi kwenye maeneo yao hayo ya kazi hivyo wakajitazame na kuleta mabadiliko .
Pia amewataka wahitimu kwenda kuwafuza na wengine namna ya kusimamia wengine ili uwekezaji huo ukalipe nakwamba ili kuleta sifa za viongozi bora mahala pakazi ni mshikamano kutoruhusu migogoro kwenye maeneo yao ya kazi.
“Hapa nataka kusema kuwa msiende kuwa vyanzo vya migogoro lakini mkawe chachu ya mafanikio kwani Mafunzo mliyopata yakaongeze malengo,chachu sehemu zenu za kazi ,”amesema.
Amesema nchi ipo kwenye mpito kutokana na kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli na kwa sasa taifa limejipanga upya chini ya Rais wa awamu ya sita Samia Hassan Suluhu.
“Niwakati wa kumuunga mkono Rais wetu mama Samia Hassan kwa kufanya kazi na kutoruhusu migogoro kwenye maeneo yenu na ninaimani kubwa mtakwenda kufanya vizuri,” amesema Profesa Ndalichako.
Ndalichako ameongeza kuwa taaisisi hiyo ambayo imeazimisha miaka kumi tangu kuazisha kwako imekuwa ni taasisi ambayo inapika viongozi na kuwafanya kutumia Mafunzo wanayopata kuleta ufanisi kwenye kazi.
Mbali ya Profesa Ndalichako pia mahafari hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo pia katika mahafari hayo wengi wao walikuwa ni watumishi wa umma na binafsi.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam