Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Kutunza mazingira ni wajibu wa kila mwananchi,hivyo jamii imehimizwa kuhakikisha inatimiza wajibu huo,kwa kutunza mazingira ya maeneo yao pamoja na fukwe za Ziwa Victoria.
Ambapo utunzaji wa mazingira unasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi,kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kuwa na mandhari mazuri ya kuvutia watalii.
Wito huo umetolewa na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam shule ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi,Bahati Mayoma wakati wa zoezi la kufanya usafi na utoaji wa elimu juu ya kutunza mazingira na urejeshaji wa taka ngumu katika mialo ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Ambapo,amewaekeza wananchi kuhakikisha hakuna uingizaji wa plastiki ndani ya ziwa hilo, utekelezaji wa shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo vya maji.
Bahati pia amezihimiza BMU kusimamia wajibu wake ikiwemo usafi wa ziwa na mazingira yake pamoja na kubainisha tafiti mbalimbali zinazoelezea juu ya namna Ziwa Victoria na mazalia yake vinavyoathiriwa na uharibu wa mazingira.
Kwa upande wake, Ofisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Jonathan Nyabugumba,amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha maeneo yao wanayoishi.
Pia kutunza mazingira yanayowazunguka ili kujikinga na magonjwa yanayosababishwa na uchaguzi wa mazingira kama vile kipindupindu na magonjwa ya tumbo.
Ambapo ameeleza kuwa ni wajibu wa wananchi kuyatunza mazingira siyo mpaka wasimamiwe na Serikali huku akiwasisitiza mawakala wa usafi kutekeleza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi.
“Nawashukuru wadau wa mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, Arena recycling na Emedo ya jijini Mwanza,wananchi endeleeni na utamaduni wa kufanya usafi hata baada ya taasisi hizi zinazotoa elimu ya mazingira kumaliza muda wao wa kazi ndani ya Ilemela,”ameeleza Jonathan.
More Stories
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania