Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Kigamboni
KAMPUNI ya Wahenga Aluminum iliyopo Kinyerezi imechangia asilimia 50 ya ujenzi wa Jengo la nyumba ya Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Dar es Salaam iliyopo Wilayaji Kigamboni .
Akitoa ahadi ya kuchangia gharama za Ujenzi Wilayani Kigamboni Mkurugenzi Kampuni ya Wahenga Aluminum John Ryoba , mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu CCM Taifa Daniel Chongolo, wakati wa kuweka jiwe la Msingi la Ofisi ya CCM WIlaya Kigamboni na Nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
“Leo ni siku ya kwanza kukutana na viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM nyumba za Dar es Salaam zote zimewekwa Aluminum na KAMPUNI yetu ya Wahenga ,Wahenga Aluminum tumesaidia Kata ,Wilaya na Mkoa kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya kujenga chama Cha Mapinduzi CCM ,Kampuni yetu itasaidia kuchangia gharama za Ujenzi wa milango ya Aluminum na madirisha tutachangia asilimia 50 ya ujenzi sawa na shilingi milioni 4.8 “amesema Ryoba
Mkurugenzi wa Wahenga John Ryoba amesema atashirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya kujenga Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumsaidia RAIS Samia Suluhu Hassan ,katika utekelezaji wa Ilani ya Chama .Ryoba alisema yeye ni kada wa chama Cha Mapinduzi CCM anashirikiana na chama na Serikali katika kuleta maendeleo .
Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi amesema atachangia shilingi milioni 5 gharama za Ujenzi huo pia atakuwa Mshauri Mkuu katika maswala ya Ununuzi wa vifaa vya ujenzi huo .
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilayani Ilala kutoka Jumuiya ya Wazazi George Mtambalike amesema ataleta miti Kwa ajili ya utunzaji MAZINGIRA ya nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam .
Aliyekuwa Waziri wa Utumishi Hawa Ghasia amesema atachangia vifaa vyote vya umeme vya jengo hilo mpaka likamilike.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato