Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewapongeza Wahariri wa vyombo vya habari nchini kwa kazi nzuri ambayo wameendelea kufanya ya kuhabarisha Umma bila ya ubaguzi.
Amesema, kutokana na weledi na ustadi wa utoaji wa taarifa kwa Umma, kumesaidia kuendeleza na kudumisha amani nchini.

Balozi Nchimbi ameyasema hayo, wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini, kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), uliofanyika leo Aprili 4, 2025 mjini Songea, ambapo amesema vyombo vya habari kupitia Wahariri wake ndiyo watu wanaoweza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wapenda amani katika kulifikisha Taifa sehemu sahihi.
“Katika mtangamano na utulivu wa nchi yetu wahariri wa vyombo vya habari ambao nyinyi ndio mnao ruhusu habari yoyote itoke kwenye chombo chako Cha habari..kama mngetumia nafasi zenu vibaya katika miaka yote mliyofanya kazi inawezekana kabisa nchi yetu isingekuwa kama hivi ilivyo leo.
Wahariri wa vyombo vya habari kwa mfano wakiamua kutengeneza msongo wa mawazo kwa raia..wanatengeneza, maana hata ukiamua kumuandika mtu mmoja tu kila siku kuwa leo kwajikwaa alipokuwa anaenda sokoni, leo kamtukana mtoto wake, hiyo maana yake unamtesa mtu katika maisha yake ya kila siku, lakini pia mnaweza kukuja jambo kutoka kuwa dogo na likaonekana kubwa katika Taifa, pia mnaweza kuchochea jambo. Lakini Wahariri ndiyo chujio la habari zote katika Taifa hivyo katika siku ambazo mmetimiza wajibu wenu mpaka sasa mmefanya Taifa letu limekuwa na utenganano”, amesema Balozi Nchimbi.
Amesema, ni dhahiri kuwa wahariri kupitia waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika kuendeleza ustawi wa nchi.

More Stories
Polisi Mbeya yajivunia miaka minne ya mafanikio
NCHIMBI: Nia ya CCM ni kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini
Balozi Nchimbi: Uchaguzi upo palepale hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia