Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 13 wa kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),unaolenga kujadili mada mahsusi huku Kauli mbiu ya mkutano huo ikiwa ni ‘Nafasi ya vyombo vya habari katika matumizi ya gesi kwa ajili ya kulinda misitu’, Mkutano huo.ambao utafanyika kesho
utashirikisha wahariri 150 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Akizungumza Aprili 28 jijini Dodoma na waandishi wa habari Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TEF, ambaye pia ni mhariri wa gazeti la FAMA Neville Meena amesema kuwa mkutano huo utafanyika jijini hapa kwa muda wa siku mbili.
Meena amesema kauli mbiu hiyo inayoongoza katika mkutano huo itatumika kama mada kuu
na kwamba kutakuwa na watoa mada mbalimbali za kitaaluma ikiwamo ya wanawake na uongozi katika vyumba vya habari, nafasi zao wajibu wao pamoja na uzingatiaji wa taaluma.
“Tupo Dodoma tunajambo letu la kitaaluma ambalo litafanyika kesho jumatatu (leo), na kesho tutakuwa na mkutano kitaaluma wa 13, namada nyingine itakuwa ni kuhusu uchaguzi kama tunavyofahamu mwaka huu tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani tukijaaliwa tutakuwa na uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani” amesema Meena.
Amesema watakuwa na mada hiyo kwa kuwa wanahusika na kuandika habari ikiwa ni pamoja na kuelekeza akili zao katika suala la uchaguzi huku akisema mada nyingine ni jinsi gani ya ufanyaji kazi kwa kuzingatia teknolojia inavyokua katika vyombo vya habari na watakavyokabiliana na Teknolojia ya akili Mnemba.
“Vyombo vyetu vya habari haviwezi kufanya kazi pasipo kuzingatia mabadiliko makubwa ya teknolojia,ule utawala wa magazeti, wa runinga kufikiria kila kitu kwamba bila wao kutanzangaza hakuna kitakachotokea, vyote hivyo vitaendelea kuwepo lakini tuzingatie teknolojia imekua kuna mitandao ya kijamii inafanya kazi,” amesema.
Naye mjumbe wa kamati hiyo Salim said Salim amesema kuwa waandishi wengi wanafanya habari za kiongozi fulani kapanda miti huku akisema wanandishi hao hawafuatilii maendeleo ya miti hiyo.
Pia aliwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa ueledi bila kuegemea upande mmoja na badala yake kuandika zile zinasoigusa kijamii.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri wa Habari Mawasoliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria