January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahakikishiwa usalama siku ya kupiga kura

Ashura Jumapili TimesMajira Online, Kagera

Jeshi I la polisi mkoani Kagera limewahakikishia wananchi usalama siku ya kupiga kura Novemba 27,mwaka huu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kipindi hiki cha kampeni ambacho zoezi linatarajiwa kuhitimishwa Novemba 26,2024.

Hivyo Jeshi hilo limewataka wananchi kuwa huru katika kipindi chote cha kampeni na upugaji kura.Kwani Jeshi hilo limepokea magari matano yatakayosaidia kuongeza utendaji kazi na nguvu,siyo tu kwa zoezi linaloendelea la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bali hata mazoezi mengine yanayoendelea baadaye kuhakikisha Kagera inakuwa salama.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari Novemba 25, mwaka huu,mkoani humo amesema kuwa, Novemba 27, mwaka huu utafanyika uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo akawahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa amani kwani mazingira ya Mkoa huo ni salama.

Chatanda, amewataka Wananchi waitumie haki yao ya msingi ya kupiga kura kwani jeshi hilo limejipana vizuri.

“Naamini uchaguzi utafanyika salama na hata baada ya uchaguzi Kagera itaendelea kuwa na amani,barabara zitaendelea kuwa salama kwani siku chache zilizopita tulipokea gari kwa ajili ya doria,”amesema Chatanda.

Aidha, amewatakia uchaguzi mwema wenye amani watanzania hususani wa Mkoa wa Kagera,kuwataka waitendee haki haki yao ya kidemokrasia ya kuwachagua wale watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo katika serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.