Na Penina Malundo
IDADI ya wagonjwa wa Corona hapa nchini imeongezeka hadi kufikia 147 baada ya jana Waziri wa Afya, Maendeleao ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kutangaza wagonjwa wapya 53 ambao wamethibitika kuwa na Corona nchini Tanzania huku mtu mmoja akifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Wagonjwa hao wamebainika baada ya upimaji wa sampuli katika maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii jana Aprili 16 na leo zionesha wagonjwa hao 53 ambao wote ni Watanzania.
Kati ya wagonjwa hao wapya, 38 wapo Dar es Salaam, 10 Zanzibar huku Kilimanjaro, Mwanza, Pwani, Lindi na Kagera kukiwa na mgonjwa mmoja mmoja huku idadi ya waliofariki ikifika watano.
Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa, asilimia kubwa ya wagonjwa hao hali zao zinaendelea vizuri isipokuwa wagonjwa wanne.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi