March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wagombea Urais  NRA wachukua fomu INEC kwenda kusaka wadhamini mikoa 10

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

MGOMBEA wa Urais na Mgombea mwenza  kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Hassan Almasi na Ally Hassan wamekuwa wa pili kuchukua fomu ya kuombea Urais katika Ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchuguzi jijini hapa leo Agosti 9,2025.

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu Almasi amesema kuwa kinachofuata sasa ni kazi ya kwenda kutafuta wadhamini kwenye Mikoa 10 na baada ya hapo kazi inayofuata ni kazi ya kuongea na wapiga kura wa nchi hii.

Huku akitaja matumaini yao matatu katika safari hiyo ya uchaguzi ambapo ametaja
Cha kwanza ni Mungu,

“Maana yeye ameshika uhai wetu na mamlaka yetu,”amesema.

Cha pili ametaja kuwa ni wapiga kura kwani kwa mujibu wa katiba wanamalamka ya kuweka uongozi .

Na cha tatu ni Mtangazaji wa matokeo ambaye ni Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

“Hayo ndiyo matumaini makubwa ambayo tunatarajia yatatuvusha hapa tulipo,”amesema.

Pamoja na hayo amesema Chama chao kinasema  Taifa kwanza vyama baadae.

“Sisi tuko tayari kukosa uongozi endapo hatutaupata lakini nchi ibaki salama,hatuna sababu ya kuingiza nchi katika machafuko kwasababu ya uchaguzi baada ya uchaguzi kuna maisha na watanzania ndiyo wakuweka uongozi katika nchi hii na ndiyo maana nimetaja vitu vitatu nchi wapiga kura na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambao ndiyo wanatangaza matokeo,”amesema.

Wagombea hao walifika katika viwanja vya Ofisi hiyo 7:55 wakiwa katika gari lenye namba za usajili T 964 ECB Benz pamoja na T 497 DNR  aina ya Murano.