January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wagombea na Viongozi wa siasa watakiwa kulinda amani na utulivu

Na Irene Clemence, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya siasa Nchini, John Shibuda amewasihi wagombea na viongozi wa vyama vya siasa nchini kulinda amani na utulivu uliopo kwa sasa kwani ni tunu za taifa

Pia amewataka kuacha kufanya siasa za chuki zinazoweza kupelekea kuvuruga amani na Umoja kwa watanzania.

Shibuda ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema siasa za chuki uamsha mitazamo hasi katika jamii na kupelekea kuvuruga umoja ulipo.

“Nawaomba wagombea wote epukeni kujenga upotofu katika jamii wakati wa kunadi sera zenu kwa kutumia lugha zinazoweza kuamsha mitazamo hasi na kusababisha mmomomyoko unaoweza kuzaa maporomoko makubwa”amesema Shibuda

Na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kujiajiri ajira za kutenda malumbano ya dhima ya kujenga kuundika kwa hasama na visasi kwani maovu yeyote hayana hazina ya burudani bali uovu huunda mikasa ya nongwa kwa vizazi vipya.

Amesisitiza kuwa wagombea wanapaswa kueshimu mfumo ulipo wa vyama vingi kwani upo kwa manufaa ya kujenga menejimenti bora ya kuiletea nchini maendeleo.

“Kila mgombea anapaswa kujifanyia ukaguzi wa kujenga na kujisahihisha dhidi ili asiwe chanzo cha mumomonyoko wa kuzaa kauli zenye mporomoko kwa usalama wa timu za taifa” amesisitiza Shubuda.

Aidha amemtaka kila mgombea kudhibiti miemuko inayoweza kujenga mlipuko wa kuunda hasira chuki na viburi vya kuchokonoa Jeshi la Polisi.

“Siasa ovu na zana potofu huunguza amani, umoja na taifa kuwa nchi ya jamii moja, ikumbukwe kuvunja amani ni rahisi sana na pia ni ngumu kurejeshwa “amesema

Shibuda amesema wanasiasa na wagombea pamoja na vyombo vya dola vinapaswa kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kuwa uchaguzi utakuwa wa haki,usawa na uwazi.

Katika hatua nyingine Shibuda amevitaka vyombo vya dola kudumisha weledi unaotekelezeka kama kinga ya kulinda urithi wa vizazi na vizazi wa usalama wa tunu.

Akizungumza kukatwa kwa wagombea wa vyama mbalimbali Shibuda amesema kuwa, tume ya uchaguzi inatakiwa kujua kuwa baadhi ya maeneo kumefanyika sintofahamu za kutengenezwa na ngazi za chini juu ya wagombea ambao wamekatwa.

“Ufatiliaji wangu haina kitengo cha upelelezi kwahiyo haina uhakiki kwa viarifu vinavyopokea hivyo ni vizuri kama tume ikatambua kuwa suala hili limewaangusha,” amesema Shibuda