January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wageni kutoka ndani ya nchi na Ulaya waridhika na Usalama Mkoa wa Arusha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha mheshimiwa John Mongella ambaye ni mwenyekiti wa Usalama Mkoani humo amesema kuwa thathimini iliyofanyika imebaini kuwa wageni wengi wanaridhika na Usalama wa Mkoa huo ambao no kitovu cha utalii hapa nchini.

Kauli hiyo ametoa jana usiku katika hafla ya Polisi day ambapo amewapongeza askari waliofanya kazi vizuri zaidi na kutoa huduma bora Kwa wananchi wanao litegemea Jeshi hilo.

Ameongeza kuwa katika Mikoa iliyopo hapa nchini Mkoa wa Arusha umeonyesha hali ya usalama kuhimarika Mkoani humo huku akiwataka askari kuendelea na utaratibu wa kupongezana kutokana na Juhudi kubwa ambazo wanafanya za kuimarisha ulinzi kitendo kilichopelekea Mkoa huo kuwa shwari.

Mongella amebainisha kuwa wageni wa ndani na wale wanaotoka mataifa ya Afrika na Ulaya wameonyesha kuridhishwa na Usalama na utulivu wa jiji hilo na Mkoa wa Arusha Kwa ujumla.

Pia Amewataka askari wao kujikita katika kutoa elimu katika jamii sambamba na dhana ya Polisi jamii na namna bora ya ushirikishwaji jamii Ili kubaini na kutanzua uhalifu katika Mkoa huo ambao no kitovu cha utalii hapa nchini.

Sambamba na hilo amewataka askari hao kufuataratibu za Jeshi hilo huku akiwataka wale wenye Mapungu yanayolichafua Jeshi kujirekebisha ili kuishi katika misingi ya Jeshi hilo.

Nae kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa hafla hiyo ni utaratibu wa Jeshi la Polisi kila mwaka wa kuukaribisha mwaka na kuuaga mwaka ulioisha huku akibainisha kuwa zoezi hilo linaenda sambamba na kuwapongeza askari waliofanya vizuri zaidi.

Nae Mdau wa Maswala ya utalii bwana Henry kimambo licha ya kulipongeza Jeshi la Polisi amesema sekta ya utalii Mtaji wake mkubwa katika biashara hiyo ni amani na utulivu ndio kitu kikubwa kinavutia watalii wengi.

Robert Mitego ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Polisi ameshukuru Kwa kustaafu salama katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi huku akiwataka askari wanaobaki kufuata misingi ya Jeshi hilo Ili kufikia hatua ya kustaafu wakiwa salama.