December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafugaji watakiwa kuwafichua madaktari vishoka wa mifungo

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

WAFUGAJI wa mifugo nchini wameshauriwa kuendelea kuwafichua madaktari vishoka kwa kutoa taarifa zao kwa Baraza la Veterinari Tanzania ili kuondoa hudum hafifu ya afya ya mifugo, isiyokidhi viwango kwa lengo la kuongeza tija katika ufugaji.

Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dodoma na Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt. Bedan Masuruli, alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

Amesema Baraza lake linaendelea kuwasaka vishoka waliojiingiza kutoa huduma ya afya ya mifugo kwa kushirikiana na wafugaji,vyombo vya habari na wadau wengine.

Dkt. Masuruli ambaye pia ni Msajili amevishukuru vyombo vya habari kwa jinsi vinavyoendelea kusaidia kubainisha uwepo wa vishoka hao, ili kuwanusuru wafungaji kuingia katika mtego ya vishoka.

Dkt. Masuruali ameendelea kutoa tahadhari hiyo kufuatia taarifa iliyotolewa na gazeti hili wiki mbili zilizopita kuhusu mfugaji aitwaye, Hassan Pixels ambaye kondoo wake 19 walikufa kwa siku moja baada ya kuzidishwa dozi ya dawa ya minyoo.

Kufuatia vifo hivyo mfugaji huyo alifikisha malalamiko yake kwenye Baraza la Veterinari Tanzania.

Mlalamikiwa anayedaiwa kuwa ni daktari kishoka (jina linahifadhiwa), alipohojiwa na Majira jana, alikiri kondoo hao kufa akisema vilitokea kwa bahati mbaya.

Amesisitiza kwamba hali kama hiyo inaweza kumtokea kwa daktari yeyote wa mifugo.

“Mimi si daktari kishoka, nilipita mafunzo lakini sikupata cheti cha udaktari na sijasajiliwa, lakini nina ufahamu wa kutibu mifugo kwa vile nina ujuzi wa kufanya hivyo na si kila daktari ana cheti.” alisema.

Kutokana na melezo ya kishoka huyo Msajili wa Baraza la Veterinari alipohojiwa, alisema maelezo ya kishoka huyu ni ya uongo na hayana ukweli wowote, kwa sababu kwa sababu amesomea uhimilishaji wa ng’ombe na siyo matibabu ya wanyama hao.

Hivyo alimtaka kishoka huyo kujitokeza kwenye Baraza la veterinari kama vile alivyojitokeza kwenye gazeti hili kwani mchakato wa kumtafuta umeshaanza ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.

Msajili huyo aliendelea kusema kuwa Baraza limekuwa likimtafuta kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio. Aliwataka wafugaji kusadia mchakato wa kumpata mlalamikiwa ambaye ni mkazi wa Kisesa Jijijini Mwanza ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Dkt.Masuruli alisema kuwa baada ya kupata malalamiko ya Hassan Pixels kuhusu vifo vya kondoo wake 19, Baraza la Veterinari lilifanya uchunguzi ili kupata ukweli na sababu ya vifo hivyo ns ilibainika kupitia uchunguzi wa kimaabara kuwa kondoo hao, walikufa kwa kupewa dozi kubwa ya dawa, kuliko inavyostahili.

Kuhusu uhalali wa kishoka huyo kutoa tiba kwa mifugo, Msajili wa Baraza alisema mtu huyo ni kishoka na anapaswa kuacha mara moja kujihusisha kutoa huduma ya afya ya mifugo kwa mujibu wa katazo la Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alilolitoa Julai 6, mwaka huu na vilevile kwa mujibu wa Sheria ya Veterinari (SURA 319)