Na David John, TimesMajira Online
Mkurugenzi wa kiwanda cha Mother Daily Full Manyonyo kilichopo wilayani rufiji Mkoa wa Pwani, Ramadhan Nyarando amesema kitendo cha kuhamishwa kwa wafugaji wilayani humo kutaleta shida kwenye eneo lake la uwekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari, Nyarando amesema kiimsing unaposikia wafugaji wanafukuzwa ni dalili ya kiwanda kufungwa kwa maana bila malighafi huwezi kukiendesha.
Amesema, ni vyema wanaotoa maamuzi kwamba wafugaj waondoke wakaangalia uwekezaji ambao umefanyika kwenye kiwanda hicho, kwasababu Rais Dkt Magufuli ameendelea kutamka anafanya maendeleo kwa pesa za ndani, hivyo lazima watambue kuwa pesa hizo zinatokana na uwekezaji wao.
Nyarando amesema, wafugaji walipotoka Ihefu waliletwa Kusini, na walipofika hapa hawakuwa na soko la maziwa, hivyo uwekezaji huu ulisaidia wafugaji kuwa na soko la uhakika la kuuza maziwa, wakati huo huo wananchi wa Rufiji kuwa na uhakika wa kupata maziwa lishe yanayotoka kwenye kiwanda hicho.
“Tunajua ilani ya CCM kwa sehemu kubwa imejikita katika kujali makundi mbalimbali yakiwemo ya ufugaji, lakini kwa hali ilivyo ni kama vile kuna baadhi ya watu wanaichezea ilani ambayo pia inazungumzia uwekezaji nchini kwa watanzania kujenga viwanda kwa maendeleo ya taifa ,” amesema Nyarando.
Kwa upande wake Ally Makene ofisa uzalishaji, na mtalaam wa kiwanda hicho amesema, tangu kuazishwa kwake walikuwa wanazalisha lita 3500 kipindi cha Januari lakini kwa sasa lita1500, hali hiyo inakwenda kuathiri uzalishaji, inakwenda kuathiri wafanyakazi, badala ya kuongeza itabidi wapunguzwe.
“Nilitegemea hao watu wakae vizuri, watoe uamuzi mzuri ambao utaleta maendeleo , uwekezaji wa kiwanda mara nyingi wananchi huwa wananufuka, kiwanda kinanufaika na serikali nayo inanufaika kwa kupata kodi,” amesema.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu