Judith Ferdinand,timesmajira,Online,Mwanza
WAFANYAKAZI wanatarajia matumaini makubwa kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kupandishwa madaraja, misharahara na kuteteta maslahi ya wafanyakazi kwa ustawi wa maendeleo ya wafanyakazi na taifa kwa ujumla.
Wakizungumza kwa wakati tofauti,wafanyakazi hao walio shiriki maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza,akiwemo Frank Chalamila wamesema,wanatarajia Rais atasimamia Sheria ya Ajira na Mahusiano.
Chalamila amesema pia wanatarajia Rais atashughulikia madeni ya wafanyakazi yote ili yalipwe,kuongeza mishahara na kuwapandisha madaraja wafanyakazi,kudumisha mahusiano ya nchi yetu na nchi nyingine,kuimarisha uongozi,
kusimamia misingi ya haki, Sheria kwa mujibu wa Katiba pamoja na kujali kundi la wafanyakazi.
Kwa upande wake Husna Hassan amesema,wanatarajia Rais atatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi ili kuboresha utendaji kazi wao kwa maslahi ya maendeleo ya taifa.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais