December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabiashara watatu wapandishwa kizimbani kwa kukutwa na madawa ya kulevya

Na Irene fundi, TimesMajira Online

Wafanyabiashara watatu Mkoani Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu Kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin kg 21.67.

Shitaka hilo limesomwa leo katika mahakama ya hakimu mkaazi kisutu na wakili wa selikali Tumaini maingu mbele ya Hakimu mkazi Mkuu Amiri Msumi na wakili upande wa utetezi Abdulahi Abdulazizi.

Wakili Maingu amedai kuwa washitakiwa wanatuhumiwa kwa kosa Moja la kujihusisha na madawa ya kulevya aina ya heroin hydrochloric.

Wafanyabiashara hao ni Ramadhani Shabani Gumbo(25) mkazi wa Ilala,bungoni ,Fahadi Nassoro Salehe(24) mkazi wa Ilala bungoni, Ashiraf Mohamed Hamisi (26) mkazi wa Sinza.

Katika hati ya mashitaka imeeleza kuwa mnamo Julai 13 mwaka 2019 katika maeneo ya mbezi gwembe ndani ya Wilaya ya kinondo mkoani Daresalaam watuhumiwa walikuwa wakifanya biashara ya madawa ya kulevya aina ya heroin hydrochloric 21.67.

Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu mashtaka hayo kutokana na kiwango Cha madawa kuwa kikubwa.

Maingu amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanasubiri mabadiliko ya hati ya mashitaka hivyo ameiomba mahakama tarehe nyingine kwaajiri ya kupisha kukamilishwa kwa usajiri wa kesi.

Wakili wa utetezi Abdulazizi ameomba upande wa mashtaka kutekeleza wanachokiaidi kwani shahuli hilo sio jipya katika mahakama hiyo.

Kesi hiyo ya kujihusisha na madawa ya kulevya imehairishwa hadi machi 14 mwaka huu kwaajiri ya kutajwa.