Penina Malundo,TimesMajira Online
WAFANYABIASHARA nchini wametakiwa kujifunza kuhusu uendeshaji wa biashara kutokana na Dunia kwenda kwa kasi itokanayo na teknolojia hivyo lazima wajifunze ili kujua taarifa muhimu za kibiashara.
Hayo yamesema Kaimu Meneja wa Uendeleaji wa Bidhaa Tantrade, Masha Hussein kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maalufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’.
Amesema, Tantrade ipo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara hivyo kikubwa ni lazima wakubali kujifunza ili kuweza kuona dunia inakwendaje na kuna nini katika sekta ya hiyo ya bishara.
“Ifike mahala sasa wafanyabiashara wetu lazima wakubali kwamba Dunia inakwenda kasi mno na kila kitu kipo kwenye digitali hivyo kuna haja ya kujifunza na nakuona wengine biashara wanafanyaji ili kuweza kuleta tija katika biashara wanazozifanya nasisi kama wasimamizi tupo kwa ajili ya kuwapa elimu na miongozo,” amesema Masha.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wajasiliamali nchini TWCC Mercy Silla, amesema kuwa, ni muhimu kwa wafanyabishara kuhudhulia mikutano ya ana kwa ana ambayo inaandaliwa na mamlaka ya biashara iliyo chini ya wizara ya viwanda Tantrade ili kupata uewelea zaidi kuhusu masoko na mahusiano ya kibiashara,
Amesema, zipo changamoto za masoko kwa baadhi ya wafanyabishara kwa kutokujua namna ya kutapata hivyo kama watapata wasaa wa kuingia kwenye mikutano hiyo watajifunza mambo mengi yanayohusu biashara na fursa zake.
“kimsingi maonyesho hadi kufikia leo yanaakwenda vizuri na kama mnavyoona hapa kumechangamka na kikubwa wanawake wamejitokeza sana katika maionyesho haya jambo ambalo linaleta faraja hususani kwenye sekta ya biashara hapa nchini,” amesema Mercy.
Pia amewataka wanawake kujitahidi kuboresha bidhaa zao hususani kwenye vifungashio ili kuleta ushindani katika eneo hilo la biashara kwa kutambua kuwa ushindani ni mkubwa mno ili lazima kujitangaza kwa kuwa na bidhaa zilizofungashwa vizuri.
More Stories
Wananchi wa Ikuvilo watakiwa kujitokeza kuhakiki taarifa zao
Watanzania wahimizwa kutenda mema
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?