Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Wafanyabiashara wadogo na wakati wilayani Ilemela mkoani Mwanza wameoimba Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), kuendelea kutoa elimu ya Miliki Bunifu kwani wengi wao hawana elimu hiyo na wanaishia kusajili jina la biashara lakini hawajui kuwa kuna kusajili alama na nembo za biashara zao.
Hayo wametaeleza kwa nyakati tofauti katika mafunzo ya Miliki Bunifu yaliotolewana BRELA kwa wafanyabiashara hao wa Wilaya ya Ilemela Novemba 14,mwaka huu yaliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Nuru Ramadan ameeleza kuwa wamejifunza mambo mengi kwani wafanyabiashara hawajui namna ya kusajili nembo za biashara.
“Tukisha sajili kampuni zetu tunasema biashara imeisha kumbe kuna kitu kingine ambacho unapotengeneza biashara yako ukaiwekea nembo lazima uende BRELA uisajili, suala hili tulikuwa hatulijui wala kilifahumu hivyo tunawashukuru hivyo tunaomba wawe wanatoe elimu hiyo kila wakati,”amesema Nuru.
Nuru ameeleza kuwa kabla ya kupata elimu changamoto ambayo wanaopitia wafanyabiashara ni kuwa mtu anaweza kutengeneza bidhaa akaweka nembo mtu mwingine tayari anayo biashara hiyo hivyo ata katika kuuza inakuwa shida yote ni kwa vile walikuwa hawajui taratibu.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Joasamwe Fauzia Ibrahim, ameeleza kuwa anashukuru kwa sababu wamepewa muongozo na BRELA ya namna ya kusajili alama kwani awali walikuwa hawana elimu hiyo.
“Kuna gundi inayozalishwa china na nyingine hapa kwa sababu hatuna alama tunatumia nguvu kubwa kujitangaza kwenye biashara hivyo kutokana na elimu tulioipata leo tutasajili alama ya biashara yetu na kuweza kujitambulisha sokoni,”ameeleza Fauzia.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji shirika la Thamani ya Mwanamke Tanzania(TMTz) Nyamumwi Lumambo, ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo ataenda kuwa balozi kwa wanawake wenzake atawaelekeza kadri atakavyoweza kwani changamoto ni kuwa watu walikuwa wanakutana na bidhaa zenye nembo yenye jina lao.
“Nimejifunza kuwa wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa ni muhimu kusajili biashara zao na nembo za biashara zao ili wawe salama na sehemu sahihi za bidhaa zao kuuzika hivyo BRELA izidi kutoa mafunzo haya kwa ukubwa na kuwafikia wajasiriamali hasa wadogo,”amesema Lumambo.
Naye Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Elizabeth Swagi ameeleza kuwa mafunzo hayo ni mazuri kwani mara nyingi wafanyabiashara wamekuwa wakipeleka malalamiko kuwa kuna watu wanabidhaa na nembo kama zao.
“Lakini ukiwauliza kama alama yako umeisajili anauliza kwani wanasajili wapi leo kupitia mafunzo haya yaliotolewa na BRELA yatawasaidia na wataenda kuwa mabalozi kwa wenzao kwani wafanyabiashara takribani 60 wameshiriki kwa kiasi fulani itaondoa changamoto hiyo na sasa wanatambua umuhimu wa kusajili biashara,”amesema.
Swagi ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kusajili biashara na alama za biashara hivyo wafanyabiashara wote wafike BRELA wanasajili ili kitu kiwe cha kwake chenyewe.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu