Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kongamano la Biashara baina ya Makampuni ya Tanzania na Waagizaji Bidhaa kutoka Korea- KOIMA lililoangazia kuimarisha ushirikiano yakinifu wa biashara kwa kuzingatia Maendeleo ya Biashara na Uchumi baina ya nchi hizo mbili.
Dkt. Latifa Khamis Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade akizungumza kwa upande wa Tanzania ameainisha mambo mbalimbali ikiwemo, kuhamsisha wafanyabiashara wa Tanzania kuchukua fursa za Biashara zinazohitajika Korea.

Amesema Makampuni 15 yaliyokuja nchini ni makubwa na ununua bidhaa zenye ubora na kiwango cha juu zenye thamani ya zaidi ya USD milioni 700 kwa mwaka.

Khamis ametoa rai kwa wazalishaji wa Tanzania kuhakikisha wanasajili bidhaa zao na alama rasmi ya Made in Tanzania ili kuweka urahisi kufanya biashara kwenye masoko ya kimataifa.

Aidha Khamis amewakaribisha na pia Wafanyabiashara hao kushiriki kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), kwa Kutangaza bidhaa za kilimo ambazo ni Made in Tanzania, hususan kahawa na bidhaa nyingine, ili kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinatambulika vyema kwenye masoko ya Korea.
Nchi hizi mbili zinafanya biashara katika sekta za Kilimo, Madini, Pamba, Mchele, Korosho, vipodozi, Teknolojia.
Aidha, kupitia Kongamano hilo Tanzania na Korea zimeingia mkataba wa makubaliano ya Biashara kupitia Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na (Korea Importers Association- KOIMA) ili kushirikiana kibiashara. Kongamano hilo limezinduliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mahmoud Thabit Kombo na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi