Na Esther Macha,TimesMajira,Online , Mbeya
WAFANYABIASHARA katika soko la uwanja wa ndege wa zamani wamemuomba Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson kusogezewa huduma za daladala katika eneo hilo ili kuwaondolea usumbufu abiria.
Hayo yamesemwa jana na wafanyabiashara hao baada ya kutembelewa na Mbunge huyo na kuongea wafanyabiashara,Wamiliki wa Mabasi na Maafisa Usafirishaji ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Jiji la Mbeya.
Aidha wafanyabiashara hao wamemuomba Mbunge huyo kuendelea kufanya biashara maeneo mengine wakati eneo hilo likiboreshwa.
Awali wafanyabiashara hao waliwasilisha kero zao kwa Mbunge huyo zikiwemo za ukosefu wa mabanda ya kupumzikia abiria na miundombinu kutokana na eneo hilo kujaa maji hivyo kuwa kadhia kwa wasafiri na wafanyabiashara.
Akijibu kero hizo Dkt Tulia amesema miundombinu ya muda mrefu inaendelea kuboreshwa wakati Halmashauri ikiendelea na mchakato wa ujenzi wa Kituo cha kisasa.
Hata hivyo Dkt. Tulia amesema kuwa ili kuwaondolea kadhia baadhi ya abiria amesema kuanzia Jumatatu ijayo kituo cha Iganzo kitatumika kupakia na kushusha abiria katika muda usiozidi dakika kumi.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dour Issah Mohammed amesema kwa kushirikiana na Mbunge wananchi watarajie maendeleo makubwa kwani Mbunge ni msikivu na mchapa kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji hilo,Amede Ng’wanidako amesema kwa sasa wataboresha miundo mbinu haraka iwezekanavyo na kuhakikisha wanarekebisha miundombinu ya barabara na maji.
Katika ziara hiyo Mbunge ameambatana na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dour Issah Mohammed na Mkurugenzi wa Jiji Amede Ng’wanidako.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa