January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabiashara nchini kunufaika na chemba ya biashira ya china

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi inayojihusisha na kuwawezesha Wafanyabiasha ya Professional Exchange Platform, (PEXPLA – TANZANIA) Jenipha Japheth, amesema kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza kunufaika na uwepo wa mashirikiano ya KIbiashara baina ya taasisi hiyo na Chemba ya Biashara ya Jinhua ya nchini China, kwa kuwafungulia milango ya kuongeza wigo wa masoko yao na kukopeshwa mitaji.

Akizungumza katika kikao maaluum kati ya taasisi hizo mbili, kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika Jiji la Hangzhou nchini China, Jenipha amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina yao yanakwenda kuongeza fursa za kibiashara kwa wafanyabiasha wa Tanzania.

“Kikao hiki ni muendelezo wa taasisi yetu ya PEXPLA katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua wafanyabiasha wa dogo, wakati na wakubwa.

“Pia PEXPLA ina jukumu la kukuza mitaji ya Wafanyabiasha, ambapo kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuanza kuwadhamini wafanyabiasha hao ili waweze kuchukua mzigo kutoka kwa wazalishaji wa China kwa mkopo, na kuziuza na baadae kujisimamia wenyewe katika Biashara zao” amesema Jenipha.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo pia imeweza kutoa udhamini kwa wafanyabiasha zaidi ya 300 kwenda nchini China, kujifunza na kujionea fursa mbalimbali za kibiashara, huku ikiwakutanisha na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali katika mazungumzo ya ana kwa ana.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Jinhua nchini China, anayeshughulika na mahusiano ya Biashara na Afrika, Jin Yongming ameishukuru taasisi ya PEXPLA kwa kuonesha nia ya kuongeza wigo kwa wafanyabiasha wa Tanzania, na kuahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabiasha hao ili kufikia malengo yao.

Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA – TANZANIA) Jenipha Japheth (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Jinhua nchini China, anaye shughulika na mahusiano ya Biashara na Afrika, Jin Yongming walipokutana katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Jiji la Hangzhou nchin China
Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA – TANZANIA) Jenipha Japheth, akizungumza na ujumbe wa Chemba ya Biashara ya Jinhua ya nchini China (hawamo pichani), wakati wa kikao chao kilicholenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya wafanyabiasha wa Tanzania na China, kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika Jiji la Hangzhou China.
Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA – TANZANIA) Jenipha Japheth (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Jinhua nchini China, anaye shughulika na mahusiano ya Biashara na Afrika, Jin Yongming (kushoto), wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Jijini Hangzhou chini China.
Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA – TANZANIA) Jenipha Japheth (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Vijana ya Sayansi na Teknolojia ya Jinhua chini China, Jiang Jingwei