Judith Ferdinand, Timesmajira online, Mwanza
Baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania wamekutana katika semina ya siku tano kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa namna ya kudhibiti ajali na kuwa na usalama barabarani ili kuondokana na madhira yanayoikumba jamii ikiwemo vifo na ulemavu.
Huku Takwimu za Mwaka 2018 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO),zinaonesha mwaka 2018 kulikuwa na vifo zaidi ya 16,000, vilivyotokana na ajali za barabarani kwa Tanzania pekee.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini akizungumza wakati akifungua semina ya siku tano Novemba 27 hadi Desemba 2,mwaka huu ya Kanda ya Afrika kuhusu mpango wa usalama barabarani iliokutanisha nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Afrika Kusini,Burundi ,Rwanda Botswana iliondaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linalohusika na utoaji wa elimu ya usalama barabarani la Tanzania Safety Roads Initiatives(TARSI) inayofanyika jijini hapa.
Sagini ameeleza kuwa ajali nchini zimepungua lakini bado zinaendelea kuwepo kutokana na sababu za kibinadamu kwaio mafunzo kama haya yanatoka fursa ya kuwapa wasimamizi wa sheria na wadau wengine kuweza kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto hiyo kutoka mataifa mengine.
Ambapo ameeleza kuwa ajali za barabarani zinatokana na sababu za kibinadamu ambayo ni ya dereva mwenyewe pia kuna matatizo ya vyombo vya moto vyenyewe,uchakavu na ubovu pamoja na miundombinu kuwa mibovu.
“Ninachofarijika ni kwamba aliyeandaa mafunzo haya ni taasisi ya vijana wa kitanzania,tutapata fursa ya Watanzania kujifunza uzoefu kutoka mataifa mengine ili yale mafunzo tutakayopata tutayatumia katika utekelezaji wa shughuli za kila siku na matarajio yetu kwa semina hii tutaendelea kuboresha huduma na taratibu za matumizi ya barabara zetu na watumiaji wa vyombo vya moto,”ameeleza Sagini.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Ramadhan Ng’anzi,ameeleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu za ukanda wa Afrika Mashariki zinazotajwa kupunguza ajali za barabarani baada ya kuweka mifumo madhubuti ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara.
“Tunaendelea vizuri na tangu Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ameruhusu mabasi yasafiri usiku sasa hivi ni mwezi wa pili hatujasikia basi limepata zimetokea ajali mbili kubwa hivi karibuni na zote zimetokea mchana,tunajitahidi kuangalia kwanini ajali zimetokea mchana lakini usiku hazijatokea hivyo imekuaje usiku wameweza tunajitahidi sana ili tufikie lengo la Tanzania bila ajali inawezekana,”ameeleza Ng’anzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TARSI Maliki Barongo, ameeleza kuwa lengo ni kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
“Elimu hii tumekuwa tunaitoa kwa wasanifu wanaojenga barabara mpaka mtumiaji wa mwisho lengo ni kuhakikisha Tanzania yetu inakuwa salama kuhusiana na ajali za barabarani,”ameeleza Barongo.
Huku lengo la semina hiyo ni kubadilishana uzoefu wahandisi wa nchini hapa na kutoka nchi zilizoendelea katika usalama barabarani pia Jeshi la Polisi nchini hapa ili kusaidia kupungua au kumaliza ajali za barabarani.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo akiwemo Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji Dkt.Amon Mwasandube ameeleza kuwa barabara zinachangia kusababisha ajali kwa kiasi kikubwa pia sheria,taratibu na kanuni zinatakiwa mara kwa mara zihuishwe kutokana na teknolojia inavyobadilika.
“Sera na sheria mara kwa mara ziweze kuhuishwa kulingana na maendeleo ya dunia na kuendelea kutoa mafunzo ya teknolojia mpya kama taasisi ya VETA,NIT ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa kuhusisha masomo na mitaala iweze kuendana na wakati,” amesema Dkt.Amon.
Mkuu wa Idara ya Mipango TANROADS Mkoa Mwanza Mhandisi Magesa Mwita, ameeleza kuwa barabara wanazojenga wanazingatia suala la usalama na kuendelea kusisitiza ni kwa namna gani barabara hizo zitazingatia usalama na alama ili kulinda watumiaji wake.
“Tunajitahidi kuweka alama za barabarani maeneo yote yanayo hitajika changamoto ni kuibiwa lakini mwaka hadi mwaka uwa tunazirudishia kadri ya bajeti ya matengenezo ya kila mwaka lakini tunapaka rangi barabarani na baada ya muda zinafifia tunafanya jitihada za kurudishia ili watumiaji wa barabara waweze kuzifuata alama hizo,”amesema Mwita.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi