Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA),limetoa misaada ya vifaa saidizi kwa ajili ya kuendelea kusaidia katika zoezi la uokoaji linaloendelea, baada ya jengo la ghorofa kuporomoka eneo la Congo na Mchikichi Kariakoo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Hivyo Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu,Ummy Nderiananga amewashukuru wadau hao,Novemba 19, 2024.Ambapo amesema miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na machela 9,mashuka 100 kutoka Red Cross Tanzania, na TPA,reflectors pamoja na cover white.
Aidha alitoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchangia huku akipongeza namna zoezi la uokoaji linavyoendelea kwa kushirikiana na wadau.


More Stories
Rungwe yajenga soko kukuza uchumi kwa wananchi
Waislamu Mwanza wapokea Ramadhani kwa maandamano ya kidini
Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala,katiba na sheria yaridhishwa ujenzi soko Kariakoo