Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Serikali imewataka wadau wa sekta ya mawasiliano kuzitunza na kuzitekeza taka hatarishi zinazotokana na vifaa vya kieletroniki.
Kwani Takwimu zataka hatarishi zinazotokana na Mabaki ya vifaa vya masiliano zimekuwa zikiongezeka hali inayo pelekea hatari za kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.
Hayo aliyasema jana Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kongamano la wadau wa sekta ya Mawasiliano pamoja na watendaji wa wizara hiyo.
“Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya taka milioni7.7 za kieletroniki huzalishwa mwaka hadi mwaka”.Alisema Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia Nape Nauye.
“Hili ni tatizo kubwa linaloendelea kukua kwasababu vifaa vingi watu hawajui pa kuvipeleka matokeo yake watu wanavitupa,
Vinamdhara makubwa vingine vinaweza kugeuka sumu na kuumiza watu lakini pia kuleta madhara kwenye jamii yetu”Aliongeza.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la kongamano hilo zinazojumuisha nchi 17 zakutoka Afrika nikuona nijinsi gani za kuzipunguza taka hizo kwa kutunga sheria na miongozo ya punguza taka hizo.
“Ni muhimu tukutane pamoja na tunao viongozi wetu wamewakutanisha wadau pamoja ili tuzubgumze namna bora ya kukabiliana na jambo hili”
Alisema lengo nikuona Matakwa ya kisheria yanafuatwa katika kuteketeza taka hizo.
“Nchi za Afrika Mashariki zimekuja Tanzania ikiwa Tanzania ni mwenyeji kujadili namna yakutokomeza na kuziharibu taka za kieletroniki “.Aliongeza waziri Nape Moses Nauye.
Mkurugenzi mkuuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk Jabir bakeri amesema kuwa kwa kushirikiana nataasisi ya umoja Mawasiliano Tanzania ECO Dk Ally Simba amesema kuwa taasi hiyo kwa kushirikiana na nchi 7wanajadili namna yakudhiti taka hizo.
Alisema Taka hizo zimekuwazikiambatana na madini hatari kwa walaji na watumiaji.
“Taka hizi ni hatarishi kwa sababu zimeambata na madini hatarishi ‘”.Alisema Dk Ally Simba.
Katibu Mtendaji – EACO Ally Simba amezitaka taasisi mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu kuzifanyia tafiti taka hizo hatarishi ilikuweza kuondokana natatizo lauharibifu wa mazingira.
Aidha alisema kuna misaada ambayo inapokelewa kutoka nje ikiaminika kuwa ni misaada lakini ni vitu ambavyo vinakaribia kuwa taka hivyo moja ya mikakati waliyojiwekea ni kuzuia misaada hiyo ambayo tayari imeshaanza kuwa taka kutoingia inchini.
“Moja ya mikakati ya kikanda ni kuona vifaa vinavyotoka nje ya nchi ambavyo ni tayari vishaanza kuwa taka haviwezi kuingia kwenye nchi yetu na pamoja ili kuhakikisha taka ambazo si za msingi kuingia nchini”
Pia alizitaja takwimu za ukuaji wa taka kwa Tanzanzia ambapo alisema kwa Tanzania ndani ya mwaka 1998 taka ziliongezeka kwa tani 2000 ambapo hadi mwaka 2019 zimeongezeka na kufikia 19, 000 kwani Duniani kila mwaka taka za kielektroniki zinazoingia ni tani milioni 60.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto