Fresha Kinasa,TimesMajiraOnline,Mara.
KATIKA kuhakikisha Jimbo la Musoma Vijijini linaandaa Wasomi na Wataalamu wengi wenye ujuzi, weledi na ubora wa hali ya juu, katika nyanja mbalimbali ndani yaJimbo hilo na Taifa pia,Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Sospter Muhongo ameandaa Mijadala itakayowaleta pamoja wadau wa Sekta ya elimu ikiwa ni Mijadala yenye Mapendekezo ya kuboresha Ufundishaji, Ujifunzaji na Uelewa wa Wanafunzi Jimboni humo.
Mijadala hiyo itahusisha wataalamu akiwemo Dkt.Zabron Kengera kutoka Chuo kikuu Cha Dar es laam,Dkt George Kaangwa kutoka Chuo kikuu Cha Dar es laam na Jeff Makongo, Ubunifu Associates.
“Mfadhili wa Mijadala hiyo Chakula na usafi ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,Prof. Muhongo.” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Hayo yamesemwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo Februari 28, 2025, ambapo imeeleza kuwa mijadala hiyo imepangwa kuanza kufanyika Machi 25, 2025, Busambara Sekondari na Washiriki ni Afisa Elimu Kata 21, na Wataalamu 3. Na Machi 26, 2025, Mjadala utafanyika Busambara Sekondari Saa 3 asubuhi – Saa 6 mchana (Primary Education) na Washiriki ni Walimu Wakuu 120, na Wataalamu 3.
“Saa 8 mchana – Saa 11 jioni
(Secondary Education)
Washiriki ni Wakuu wa Sekondari 32,
na Wataalamu 3. Na Machi 27, 2025 utafanyika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Kwikonero na Washiriki ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ma-Afisa Elimu, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na Wataalamu 3.”imeeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa.
“Washiriki kutoka kwenye shule zetu zikiwemo shule za Serikali, wanakaribishwa pia Shule za Binafsi, wanakaribishwa. Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Muhongo alishafadhili mijadala yenye malengo kama haya ya Machi 2025. Mijadala hiyo ni Mwaka 2019, Mjadala wa Mkoa wa Mara, mwaka 2021 Mjadala wa Wakuu wa Sekondari za Musoma Vijijini. Tuendelee kuchangia uboreshaji wa elimu itolewayo kwenye shule zetu.” imeeleza taarifa hiyo.
Kwa upande wao Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wameiambia Majira Online kuwa, mijadala hiyo itakuwa na manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha elimu inayofundishwa inakidhi ubora na kila Mdau anashiriki vyema katika kuimarisha sekta ya elimu jimboni humo kwa kutoa mawazo chanya na kushiriki moja kwa moja kuchangia maendeleo ya elimu.
“Mijadala hii imekuja muda mzuri, ambapo shule nyingi za Sekondari zimejengwa jimboni mwetu kwa usimamizi madhubuti wa Mbunge Prof. Muhongo. Matumaini yangu changamoto zilizopo kwenye sekta ya hii kupitia Mijadala hiyo zitapatiwa majawabu na mikakati madhubuti ya kwenda kwenye ufanisi.”amesema Julius Majura Mkazi wa Nyakatende.
Naye Marco Mussa Mkazi wa Kata ya Suguti amemshukuru Prof. Muhongo kwa maono yake ya kufadhili Mijadala hiyo, amesema italeta mapendekezo chanya kwa Wadau wa elimu namna ya kushirikiana kikamilifu kuhakikisha ufaulu unapanda kwa Wanafunzi katika mitohani yao. Na pia kupata ufumbuzi wa kukabiliana na Upungufu wa Walimu wa masomo ya Sayansi jimboni humo.
More Stories
Tuzo za EAGMA zazinduliwa rasmi
Katibu Mkuu Nishati aipongeza Sweden kufadhili miradi ya umeme nchini
RAS Seneda akabidhi msaada wa Mablanketi kwa wazee na yatima