January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau LSF wafikisha elimu takribani watu mil. 6.4

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Onlinw, Dar

WADAU wa Shirika linalofanya kazi ya kukuza upatikanaji wa haki nchini kupitia Uwezeshaji wa Kisheria (LSF) wamefanikiwa kutoa elimu ya masula ya kisheria iliyowafikia watu takribani milioni 6.4.

Kati ya watu hao asilimia 45 walikuwa wanaume na asilimia 55 na asilimia 55 wakawake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaa na Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, wakati wa ufungunzi wa mkutano maalum wa siku mbili ukiwakutanisha na wadau wake ambao ni mashirika zaidi ya 200 ya wasaidizi wa kisheria nchi nzima pamoja na mashirika yanayotekeleza miradi ya upatikaji haki.

Mkutano huo unafanyika kwa njia ya mtandao. Akizungumza na washiriki wa mkutano huu, Ng’wanakilala amesema; “Tumekuwa tukifuatilia kwa karibu kazi zinazofanywa na wadau wetu. Tunatumia taarifa hizi kwa ajili ya kupanga mikakati mizuri ili kuweza kuwafikia watu wengi hasa wenye uhitaji kama vile wanawake na watoto.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza leo na wakurugenzi wa mashirika ya watoa huduma za wasaidizi wa kisheria nchini zaidi ya 200 nchini wakati wa mkutano ulioandaliwa na LSF kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kujadili masuala ya kiutendaji katika mradi wa upatikanaji haki nchini ikiwemo utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria kwa makundi yenye uhitaji kwa watu wote hususani wanawake na watoto.

Lengo letu ni kuleta maendeleo kwa kuwa tunaamini kabisa hakuna maendeleo bila haki.”

Amesema mkutano huu unafanyika mahususi kwa ajili ya kuweka mipango mikakati wa kuendelea kufanya kazi pamoja kati ya LSF na wadau wake wote wa masusala ya haki na hasa mashirika ya wasaidizi wa kisheria katika kipindi hiki cha mwaka 2021.

“Nina furaha sana kuonana nanyi leo ingawaje mko mbali, lakini kupitia teknolojia tunaweza kukutana na kujadili masuala muhimu katika mustakabadhi mzima wa upatikanaji wa haki.

Nina furaha zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wadau wetu nyinyi mmefanya kazi kubwa sana na imetupa matokeo makubwa ukilinganisha na malengo tuliyokuwa tumejiwekea.”

Meneja wa Utafutaji wa Rasilimali za Miradi ya Maendeleo na Mawasiliano wa Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde akizungumza leo na wakurugenzi wa mashirika ya watoa huduma za wasaidizi wa kisheria nchini zaidi ya 200 wakati wa mkutano ulioandaliwa na LSF kwa njia ya mtandao, kwa ajili ya kujadili masuala ya kiutendaji katika mradi wa upatikanaji haki nchini ikiwemo utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria kwa makundi yenye uhitaji kwa watu wote hususani wanawake na watoto.

Aidha, Mkurugenzi wa Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Bumbuli (BPO) Mkoani Tanga, Ramadhani Mtana, ameishukuru LSF kwa kazi kubwa ya kuendelea kutoa ruzuku kwa wadau wake na hasa wasaidizi wa kisheria kwakuwa suala la fedha limekuwa changamoto katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“LSF kama wadau wetu mkuu tunakushukuru sana kwani umekuwa mstari wa mbele kutoa mchango wako hasa ruzuku katika taasisi zetu.

Kupitia ruzuku hizi tumeweza kuhudumia wananchi wengi nchini hasa wanawake ambao wanakumbana na changamoto mbalimbali kama vile kesi za mirathi, ukatili wa kijinsia pamoja na matatizo mengine,” amesema Mtana.

Meneja wa Ufuatiliaji na Matokeo wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Said Chitung akiwasilisha mada leo wakati wa mkutano ulioandaliwa na LSF kwa njia ya mtandao, ambapo umewakutanisha wakurugenzi wa mashirika ya wasaidizi wa kisheria zaidi ya 200 nchini kwa ajili ya kujadili masuala ya kiutendaji katika mradi wa upatikanaji haki nchini ikiwemo utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria kwa makundi yenye uhitaji kwa watu wote hususani wanawake na watoto.

LSF kupitia wadau watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria mpaka sasa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita imesaidia kutolewa kwa elimu ya masuala ya kisheria, jambo lilisababisha kuripotiwa kwa matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia, ambapo asilimia 68 ya matukio yote yaliyoripotiwa yalitatuliwa na wasaidizi wa kisheria kabla ya kufikishwa mahakamani.

Asilimia 11 ya matukio yaliyoripotiwa yalipewa rufaa ya kwenda mbele kwa hatua zaidi na asilimia 17 ya matukio yaliyoripotiwa bado yanashughulikiwa mpaka sasa.

Wasaidizi wa Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Kinondoni (KPO) pamoja Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Ubungo (UPO) wakifuatilia kwa pamoja mkutano wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala na Wakurugenzi wa Mashirika ya Wasaidizi wa Kisheria nchini zaidi ya 200 unaofanyika kwa njia ya mtandao ili kujadili masuala ya kiutendaji katika mradi wa upatikanaji haki nchini ikiwemo utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria kwa makundi yenye uhitaji kwa watu wote hususani wanawake na watoto.

LSF imekuwa ikitekeleza mradi wa upatikanaji wa haki nchini katika kipindi cha takribani miaka 10, ambapo imekuwa ikitoa ruzuku kwa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma za msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria ili kusaidia watu mbalimbali hasa wanawake.