Na Holliness Ulomi, TUDARCo
KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa ameweka wazi kuwa, mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaochezwa Julai 3 ni zaidi ya fainali kwani wanahitaji kushinda mchezo huo ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa msimu huu wa Ligi Kuu.
Gomes ametoa kauli hilo baada ya ushindi wa juzi usiku wa goli 4-1 dhidi ya Mbeya City ambao umewafanya kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na alama 73 na sasa wanahitaji alama tatu pekee zitakazowafanya kufikisha alama 76.
Katika mchezo huo magoli ya Simba yalifungwa na Rally Bwalya dakika 31, Luis Miquissone dakika ya 35, John Bocco dakika ya 47 na Clatous Chama dakika ya 86 huku goli la Mbeya City likifungwa dakika ya 51 na mshambuliaji Pastory Athanas.
Magoli hayo manne yanawafanya Simba kufikisha goli 96 katika mechi 29 walizocheza hadi sasa ambapo wameshinda 23, sare nne na kupoteza mechi mbili huku yakimfanya kujivunia safu yake ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa.
Katika goli hizo 69, Bocco amefunga goli 14, Meddie Kagere goli 11, Chris Mugalu goli 10, Miquissone goli tisa na Chama kafunga goli nane ambazo jumla ni goli 52 ambazo hadi sasa hakuna timu yoyote ndani ya Ligi hiyo iliyofikisha goli hizo.
Gomes amesema kuwa, jambo muhimu kwao kwa sasa ni kuendelea kushinda hasa katika mchezo ulio mbele yao ili kutwaa ubingwa kwa msimu wan ne mfululizo jambo ambalo lilikuwa kwenye mipango yao kwa miezi miwili iliyopita.
Amesema, mchezo huo utakuwa ni zaidi ya fainali kwao na huenda wakaingia na mfumo mwingine kutokana na kiwango bora walichokionesha wachezaji wake katika mechi kadhaa zilizopita ambazo alilazimika kubadili mifumo ambayo pia imewapa ushindi.
Anachokihitaji ni wachezaji wake kumuonesha kiwango bora wanachokionesha mazoezini katika mchezo huo muhimu na hana shaka na hilo kwani kwani anaamini katika uwezo walionao wachezaji wake.
“Yanga ni timu nzuri lakini kuna mambo mengi tumeyasoma kwao katika mechi zao kadhaa zilizopita ikiwemo dhidi ya Mwadui ambayo tumeshaanza kuyafanyia kazi ili kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo wetu wa Julai 3,” amesema Kocha huyo.
Gomes amesema kuwa, hadi sasa wachezaji wake wamemdhihirishia kuwa ni bora zaidi jambo linalowafanya kutokuwa na wasiwasi wowote kuelekea katika mechi zao zilizosalia za Ligi Kuu pamoja na mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam sports Federation Cup) dhidi ya Azam.
Alisema kuwa, watatumia siku zilizobaki kuelekea katika mchezo huo kurekebisha makosa kadhaa waliyoyaona kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City ili kupata ushindi kirahisi katika dhidi ya Azam ambao wamekuwa bora mara zote wanapokutana nao.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania