December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wabunifu waaswa kuendeleza vipaji

Na Angela Mazula, TimesMajira Online.

WABUNIFU mbalimbali wa mitindo ya mavazi hapa nchini wameaswa kuendeleza vipaji vyao kwa kutumia fursa za wabunifu wengine ili kukuza tansia hiyo ya mitindo na mavazi.

Akizungumzia hilo leo, msemaji wa shindao la ‘Pop up Shop Sundowner’ Amina Lweno amesema, Jukwaa kubwa la maonyesho ya mavazi Afrika Mashariki na Kati la ‘Swahili Fashion week’, linatarajiwa kufanyika nyumbani kwa balozi wa Canada Pamela Donnel Novemba 27 mwaka huu, kuanzia majira ya saa tisa kamili mchana mpaka saa mbili usiku.

Lweno amesema, ‘Pop up Shop Sundowner’ ni fursa ya nusu siku kwa wabunifu, wafanyabiashara, wasanii na wajasiriamali kuonesha ubunifu na uhodari wao katika sanaa ya ubunifu na mitindo.

Hata hivyo amesema, fursa hiyo inawapa washiriki na wafanyabiashara fursa ya kuonyesha kazi zao na kuwapatia soko jipya kwa ajili ya kuuza bidhaa zao mbalimbali nje ya nchi.

“Fursa hii haiwapatii tu nafasi ya kuuza bidhaa na huduma zao,vilevile inawapatia pia washiriki fursa ya kukuza majina ya biashara zao na kuwaunganisha na fursa mpya,” amesema Lweno.