LILONGWE, Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera anasema juhudi za kupambana na ufisadi zitacheleweshwa nchini humo kwa sababu Bunge linakataa kuthibitisha chaguo lake la mkuu wa kuongoza Ofisi ya Kupambana na Rushwa.
Chakwera ameyasema hayo wakati akihutubia Bunge huku akionyesha kusikitishwa na kukatishwa tamaa na kamati kukataa jina la mteule wake, Martha Chizuma siku moja kabla.
Kamati ya Uteuzi wa Umma ya Bunge (PAC) ilidai Chizuma alikataliwa kwa sababu alishindwa kupata alama zinazohitajika kwa uthibitisho.
Nusu ya wabunge katika kamati hiyo walimpa alama za chini baada ya mahojiano ya tathmini, na matokeo yaliyokusanywa yalionyesha Chizuma akipata alama 15 tu kati ya 25 inayowezekana, chini ya kiwango cha chini cha kufaulu cha 17.
Rais Chakwera aliwataka wabunge, kwa maneno yake waweke kando maslahi ya kisiasa na ya binafsi na wafanye sehemu yao katika kuharakisha mabadiliko ambayo Wamalawi wameyatafuta kwa muda mrefu.
More Stories
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Samia avuna makubwa Mikutano ya Uwili G20
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho