Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
WAAMUZI kutoka nchini Angola wataamua mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kati ya wenyeji Tunisia dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ utakaochezwa Novemba 13 mjini Tunis.
Katika mchezo juo wa Kundi J, Mwamuzi wa kati atakuwa Helder Martin Rodrigues De Carvalho akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba moja Jerson Emilliano Dos Emilliano Santos pamoja na Mwamuzi msaidizi namba mbili Ivanlido Meirelles De Oliveira.
Mwamuzi wa akiba katika mchezo huo atakuwa Joao Amando Muanda Goma huku Kamisha wa mchezo huo Karam Kordy Abdel Fattah kutoka nchini Misri.
Tayari kikosi cha Taifa Stars kimeshatua nchini Tunisia baada ya kumaliza kambi yao ya siku tatu waliyoweka katika mji wa Istanbul, Uturuki.
Katika mchezo huo, Taifa Stars itamkosa Nahodha wake, Mbwana Samatta ambaye anamajeraha ya mguu, Thomas Ulimwengu ambaye watamkuta Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya marudiano pamoja na Adam Adam ambaye alibaki hapa nchini.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania