Nathaniel Limu na Seif Takaza, Singida
WAANDISHI wa habari mkoani Singida, wamehimizwa kutumia taaluma yao kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora, ili pamoja na kujikinga dhidi ya magonjwa, miili yao iwe na nguvu ya kufanya kazi halali zitakazowawezesha kujiingizia mapato.
Wito huo umetolewa juzi na Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mtega wakati akifungua semina ya siku mbili iliyoandaliwa na kufadhiliwa na Shirika la World Vision Tanzania. Semina hiyo ya siku mbili imefanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini hapa.
Amesema waandishi wa habari ni kiungo muhimu kwa kazi ya kuelimisha na kuhamasisha mambo mengi ya maendeleo, ikiwemo matumizi sahihi ya lishe. Lishe inayozingatia makundi matano ya chakula.
“Elimu juu ya umuhimu wa lishe bora ikitolewa kupitia TV, redio na hata magazeti inafikia wananchi wengi kwa muda mfupi mno. Kwa kifupi inafika nchi nzima, huo ndiyo umuhimu au faida ya vyombo vya habari,” amesema na kuongeza;
“Niwahimize kuanzia sasa tengeni muda wenu tusaidiane kuelimisha jamii iweze kubadilika na kuanza kuzingatia lishe bora, tukifanikiwa kwa hili mkoa wetu utakuwa na watu wenye afya bora na nguvu ya kufanya kazi za maendeleo”.
More Stories
Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala,katiba na sheria yaridhishwa ujenzi soko Kariakoo
TRA Tanga yakusanya bil.178.3 kwa miezi sita
Wataalam Sekta ya utalii watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu,kujituma na kuwa wabunifu