January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waandishi wahimizwa kuelimisha jamii madhara ya rushwa kwenye uchaguzi

Na Raphael Okello, Timesmajira Online,Musoma

MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Mara, Mohmed Sharif amewahimiza waandishi wa habari mkoani humo kusaidia kuelimisha jamii madhara ya rushwa katika uchaguzi

Sharif ambaye Agosti 9,2024 alikuwa akiwasilisha mada katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani Mara,amesema rushwa imekuwa tatizo wakati wa chaguzi mbalimbali nchini.

Amesema waandishi hao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanaelimisha jamii kupitia vyombo vya habari ili iepuke matumizi ya rushwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa utakayofanyika November 25 , 2024.

Aidha amesema rushwa katika uchaguzi usababisha kupatikana kwa viongozi wasio na maadili na wasioweza kusimamia vyema rasilimali ya nchi.

“Rushwa uzaa viongozi duni na wasioweza kusimamia rasilimali ya nchi hivyo huiletea nchi umaskini,”amesema Mohmed.

Pia ametaja madhara ya rushwa kuwa ni pamoja na kuwanyima wapiga kura nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowataka hali inayokwamisha maendeleo.

Pamoja na udhalilishwaji wa wananchi na jamii kwa kukosa huduma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara,Jacob Mugini amesema klabu hiyo itasimamia waandishi wa habari katika kuhakikisha kuwa wanahabarisha wanachi.

Ameitaka TAKUKURU mkoani Mara kuweka mkakati wa kuwajengea uwezo waaandishi wa habari ili wawe na uelewa wa kuchanganua taarifa za rushwa.