Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
WAANDISHI wa habari nchini wamekubushwa wajibu wao wa kuandika habari zinazochochea amani na kulinda maslahi ya taifa pamoja na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akizungumza jijini Mwanza,Machi 19,2026 wakati wa hafla maalum ya Iftar iliyoandaliwa kwa ajili ya wanahabari wa mkoa huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji wa Malori ya Masafa Marefu na Mabasi ndani na nje ya nchi, Hassan Dede,amesema kuwa jukumu la kulinda amani linapaswa kubebwa na kila mmoja, hususani waandishi kupitia kalamu zao.

Dede amesema,vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuhakikisha tunu ya amani inalindwa na kuendelezwa kwa ustawi wa taifa.
Ambapo amesisitiza kuwa anatambua mchango wa wanahabari katika kuchochea maendeleo ya mkoa wa Mwanza na taifa kwa ujumla.
Sanjari na hayo Dede amesema,lengo la kuandaa tukio hilo la Iftar ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa sekta ya usafirishaji na wanahabari, pamoja na kutoa shukrani kwa mchango wao katika kuhabarisha na kuelimisha jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Binagi Media, George Binagi, amewashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na wanahabari wa mkoa wa Mwanza,kwani ushirikiano huo umekuwa chachu ya maendeleo na umewezesha kupatikana kwa mafanikio mbalimbali.
“Ni muhimu pia kukumbushana wajibu wetu wa kijamii. Mara nyingi tumekuwa mstari wa mbele kuripoti matukio ya wengine, lakini tusisahau kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii yanayotuhusu sisi wenyewe,”amesema Binagi.





More Stories
Watakiwa kuondoa dhana potofu kuhusu chanjo ya polio
Makamba,Kanza washiriki mkutano wa Powering African Summit
Bechina atoa futari kwa wananchi 750 Ilala