Na Mwandishi wetu Timesmajira online
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema vitambulisho vya kidigitali kwa waandishi wa habari vitajenga heshima na kuwawezesha kutambulika ndani ya Nchi na nje ya Nchi.
Msigwa ameyasema hayo wakati akizungumzia na waandishi wa habari mapema leo Machi 16,2025 masuala mbalimbali ikiwemo Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita katika bandari kavu ya Kwala Mkoani Pwani .
“Wakati mwingine wadau wetu wanatukosea kwa sababu kidogo mambo yetu ayajanyooka vizuri kwaiyo tumeishatatua tatizo hili kupitia vitambulisho vya kidijitali waandishi wa habari watatambulika ndani ya nchi na nje ya Nchi”amesema Msigwa

Amesema pindi mtu atakapotaka kuthibitisha kama ni Mwandishi wa habari hata hitaji kufunua makaratasi na badala yake atakakiwa kwenda katika tovuti ya Serikali na kujua kama ni Mwandishi halali au sio halali .
Msigwa amesema vitambulisho vya kidijitali vitapunguza waandishi wa habari wasiokuwa na sifa (makanjanja), wanaoharibu tasnia ya habari.
Aidha amesema ifikapo April mwaka huu watatakiwa kutumia vitambulisho vya kidijitali.
Pia ameongeza kuwa Mfumo wa usajili kwa waandishi wa habari utazinduliwa hivi karibuni, na hivyo amewaomba waandishi kuendelea kujiendeleza kitaaluma ili wasipitwe na fursa hiyo adhimu.
More Stories
MSIGWA:Mfumo wa usajili waandishi wa habari kidijitali upo mbioni kukamilika
Kongani ya Viwanda ya Sino _Tan kutoa ajira laki moja
Mahundi awataka wanachuo kutoendekeza anasa