December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waajiri watakiwa kushirikiana na vyama vya Wafanyakazi nchini

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

SERIKALI imewataka waajiri wote nchini kuendelea kushirikiana na vyama vya Wafanyakazi ili kukuza Majukwaa ya Majadiliano ya Kijamii ili kusaidia ustawi wa jamii wenye uchumi imara mahala pa kazi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu) Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku Moja kuimarisha Uhusiano Bora kati ya Chama Cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara, Taasisi za fedha huduma na ushauri (TUICO) ambapo amesema Serikali inapenda sekta zote za kazi kwani zina mchango mkubwa kuongeza pato la Taifa.

Aidha, Waajiri watimize wajibu wao Kisheria wa kutoa nafasi kwa Vyama vya Wafanyakazi kutekeleza shughuli zake Sehemu za Kazi ikiwa ni pamoja kuhamasisha Wafanyakazi kujiunga na Vyama, kuendesha Majadiliano ya Pamoja, kutoa fursa ya Vyama kuwahudumia Wanachama wake, kuendesha Vikao vya Usuluhishi wa Migogoro ya Kikazi na Uundwaji wa Majukwaa na Mabaraza ya Wafanyakazi.

Warsha hii imetukutanisha Wadau muhimu wa Sekta ya Kazi Nchini ikiwa na Dhamira Kuu isemayo “Tija na Ufanisi ni Matokeo ya Uhusiano Bora Sehemu za Kazi”. Ni Rai yangu kuwa Warsha kama hizi zitaendelezwa sio tu na TUICO bali na TUCTA, ILO, ATE na Wadau wengine wa FES.

Naamini kuwa Washiriki wa Warsha hii tutashiriki kikamilifu katika Mafunzo, Majadiliano na hatimaye mtaandaa Mpango Kazi wa pamoja wa namna ya kuendeleza Kazi hii njema ambayo wenzetu TUICO na ATE wameianzisha.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara, taasisi za fedha, huduma na ushauri (TUICO) Paul Sangeze amesema Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi waandamizi waliohudhuria itakuwa chachu yale yatatakayojadiliwa na kuleta tija kwa kuboresha mazingira mahala pa kazi.

Kwa Upande wake Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Naomba amesema Waajiri haki ya kujiunga na Chama Cha Wafanyakazi ipo kikatiba mtu binafsi hashurutishwi anajiunga kwa hiari yake mwenyewe na anatakiwa afuate utaratibu.

Hivyo, Waajiri ni Wadau wakubwa hivyo ushirikiano huo utasaidia kutatua changamoto mahala pa kazi hivyo ni vyema mikaba yote yote ya kazi ifanyike kwa uwazi na majadiliano yafanyike Kwa Nia njema pande zote waridhike.