December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wiliam Ole Nasha (wa pili kulia) akikagua moja ya chumba cha mihadhara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua namna walivyojiandaa kupokea wanafunzi katika mazingira ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corana. (Na Mpigapicha Wetu)

Vyuo,kidato cha 6 kuanza masomo leo


Ni baada ya miezi miwili ya mapambano ya Corona, tahadhari zaimarishwa, wanafunzi waripoti, waridhishwa na maandalizi

Na Waadishi Wetu

WANAFUNZI wa vyuo na wa kidato cha sita nchini wanatarajia kuanza masomo yao leo baada ya kukaa nyumbani kwa miezi miwili kufuatia uamuzi wa Serikali wa kufunga vyuo na shule baada ya kuripotiwa wagonjwa wa Corona.

Uamuzi wa kufungua vyuo hivyo umefikiwa na Serikali baada ya maambukizi ya ugonjwa huo kupungua nchini.

Gazeti hili limetembelea vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu Muzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha SAUT pamoja na sekondaro kadhaa zenye wananfunzi wa kidato cha sita.

Katika vyo na Sekondari hizo tayari wanafunzi walikuwa wameanza kuripoti, huku hatua zote za tahadhari zikiwa zimechukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwapima joto la mwili.

Wanafunzi hao wameridhishwa na hatua za maandalizi zilizochukuliwa na vyuo hivyo kwa ajili ya kuwakinga na virusi vya Corona.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Majira wakiwa kwenye vyuo vyao, wamesema wamefurahishwa na mazingira waliyoyakuta na hivyo kuwaondoa hofu waliyokuwa wamejijengea kabla ya kufika vyuoni.

Hata hivyo waliahidi kuwa mabalozi wa mabadiliko, kwani maisha wanayotakiwa kuishi sasa ni lazima watofautiane sana na kipindi kile ambacho mlipuko wa Corona haukuwepo nchini.

“Tunashukuru maana tumekuta tahadhari zimechukuliwa, ukifika getini lazima kwanza utapimwa joto la mwili na kuna vifaa vya kunawa mikono kila sehemu, matangazo ya tahadhari; yanatolewa muda wote yakituhumiza tuvae barakoa muda wote tunapokuwa kwenye mikusanyiko,” amesema mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Mzumbe akizungumza kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini.

Uongozi wa vyuo hivyo umeliambia gazeti hili kuwa hatua zote zinazoelekezwa kwenye mwongozo wa Wizara ya Afya zimezingatiwa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (jina linahifadhiwa) amesema Chuo hicho kimezingatia miongozo yote iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya na Tume ya Vyuo Vikuu na kwamba hata Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliridhishwa na maandalizi kwenye mabweni ya Magufuli.

Katika Chuo cha SAUT, waandishi wetu wanaripoti kuwa tahadhari zote zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa wingi vifaa vya maji tiririka, sabuni, vitakasa mikono.

Baadhi ya wanafunzi walikuwa tayari wamewasili katika vyuo hivyo na wengine wakitarajia kuripoti leo kutoka maeneo mbalimbali.