Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, llala
VYAMA vya Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi (CotwuT) pamoja na chama cha Wafanyakazi wasafirishaji kwa njia ya Barabara (TAROTWU )wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusikiliza kilio chao .
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa COTWU T ,Mussa Mwakalinga ,alisema Julai 26 Mwaka huu Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu ilitoa taarifa kuhusu ilivyoshughulikia malalamiko ya Wafanyakazi Madereva kuhusiana na madai yao.
“Tunaipongeza Serikali kwa hatua waliochukua katika kushughulikia kero ,hoja na malalamiko hayo kwa pamoja tunaipa hongera kwa kuweza kusikia kilio cha wafanyakazi madereva Serikali yetu sikivu ” alisema Mwakalinga .
Mwakalinga alisema pamoja na Serikali kushughulikia malalamiko hayo lakini kuna baadhi ya hoja na malalamiko bado hayajashughulikiwa na mengine yameshughulikiwa lakini utatuzi wake bado hayajakidhi vile viwango vilivyotarajia hivyo madereva kubaki na manung’uniko .
Aidha Mwakalinga alisema kati ya malalamiko 12 ambayo wamewasilisha Serikali ni kero nne kati ya hizo hazijashughulikiwa ,Mfumo wa upakiaji mafuta depo ,malipo ya madereva wanaosafirisha sumu ,malipo kuhusu ushushaji mizigo na utaratibu na ushushaji wa vimiminika na gesi kuratibiwa Mamlaka husika za Serikali .
Wameiomba Serikali kwa utaratibu uleule uliotumika malalamiko hayo ambayo yalitolewa taarifa pia wayashughulikie malalamiko yaliobaki kwa ajili ya kuondoa malalamiko na manung’uniko yaliobaki .
Pia wameomba Serikali malalamiko ya Wafanyakazi wa madereva yafanyike kwa wakati Ili kuweza kuondoa malalamiko yao mapema.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote