Na Penina Malundo, TimesMajira Online
VYAMA 12 nchini vimekubaliana kuungana katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu katika nafasi ya Ubunge na Udiwani ambapo kila Chama kitasimamisha wagombea 22 na kuungwa mkono na vyama vingine.
Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Democratic Party( DP),Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA),Chama cha Wakulima(AFP ),Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD),Chama cha United People’s Democratic Party (UDDP),Chakancha Demokrasia Making(MAKINI) ,Chaka cha Tanzania Labour Party(TLP),Chama cha United Democratic Party(UDP),Chama cha Sauti ya Umma(SAU),Chama cha National Leque of Democracy (NLD),Chama cha Umoja wa Mabadiliko ya Demokrasia(ADC) na Chama cha Kijamii( CCK )vimeamua kushirikian kwa pamoja na kusimamisha wagombea katika nafasi ya Ubunge na Udiwani kuhusu Mgombea Urais bado vyama hivyo havijafikia muafaka katika kujadili.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama hivyo 12 visivyokuwa na wawakilishi Bungeni, Abdul Mluya amesema, wameamua kuungana kwa pamoja kutoka na na mitazamo yao kuendana kwa masuala ya kisiasa na sio kiuhanarakati.
Amesema, sasa ni wakati wa kushindana kwa sera na hoja na sio kwa rushwa hivyo vyama vinavyokemea rushwa vinapaswa kutoishia kukemea katika chaguzi za ndani pekee bali ziende moja kwa moja hadi katika uchaguzi mkuu.
Katibu wa Umoja huo, Hassan Almas amesema, anashangazwa na baadhi ya vyama vilivyolalamika kuwa vililazimishwa kusaini marekebisho ya maadili katika kikao cha wadau kwa ajili ya mjadala wa Maadili ya Uchaguzi.
Amesema, hakuna chama chochote kilicholazimishwa kusaini marekebisho hayo ila ilivyoonekana kwa baadhi ya vyama vinakosa uhuru wa maamuzi ndani ya vyama licha ya kuwa ni viongozi wakubwa.
Kwa upande wake, Mratibu wa Umoja huo, Rashid Rai amesema, vyama hivyo 12 vimejipanga kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu wa mwaka huu na watahakikisha wanapata uwakilishi bungeni.
Amesema, mara nyingi uchaguzi mkuu unakuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la rushwa hivyo viongozi wa vyama wanapaswa kusisitiza juu ya jambo hilo.
More Stories
Balozi Kombo :Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu nishati yakamilika, Marais 25 kuhudhuria
Mbunge Mavunde awawezesha kiuchumi wafanyabiashara soko la Sabasaba Dodoma
Msama: Geor Davie ni mtumishi wa kweli