Na Joyce Kasiki,timesmajira online,Dodoma
KAMPUNI ya Vodacom Foundation imezindua tovuti ya elimu iitwayo E-
fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya
ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari ambayo inafuata mitaala
ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa
bure kwa njia ya mtandao.
Lengo la Tovuti hiyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa
elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari nchini.
Akizungumza wakati akizindua tovuti hiyo katika mashindano ya Sayansi
,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021 Waziri wa Elimu,Sayansi na
Tekonolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema,kwa kupitia tovuti hiyo
wanafunzi watajifunza masomo mbalimbali wanapotumia simu za
mkononi.
“Mtandao huu utaboresha elimu kwani italeta hamasa kwa wanafunzi
kujisomea kutokana na wanafunzi wengi kupenda kutumia simu za mkononi
.”amesema Profesa Ndalichako
Aidha Profesa Ndalichako amefurahishwa na kampuni hiyo
ilivyoshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kutoa Kompyuta na
Routers kwa wanafunzi .
Waziri Ndalichako ameiomba kampuni hiyo kuongeza vitabu zaidi katika
tovuti hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi kujifunza huku akitoa rai
kwa kampuni nyingine kuiga mfano wa Vodacom Tanzania Foundation
kutumia teknolojia kusaidia jamii.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Rosalynn Mworia
amesema E- fahamu ni tovuti ya masuala ya kielimu inayopatikana
mtandaoni bure kwa ajili ya wateja wa Vodacom huku akisema kampuni
hiyo imeamua kutoa huduma hiyo bure kama sehemu ya kuunga mkono juhudi
za Serikali za kutoa elimu bila malipo kwa shule msingi na sekondari
nchini.
Amesema tovuti hiyo ina nyenzo na taarifa muhimu za kielimu kwa
ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ikijumuisha masomo
ya Hisabati,Sayansi,Sanaa na Sayansi ya Jamii.
“Ili kupata E- fahamu kwenye simu ama Kompyuta utahitaji kuunganishwa
na huduma ya mtandao wa internet ya Vodacom au kutumia WiFI ambapo
baada ya hapo mhusika ataweza kuangalia video za mafunzo ambapo
amesema maudhui yanapatikana katika lugha za Kiswahili na Kiingereza
ambapo yapo katika muundo wa sauti,video,machapisho ya PDF na mazoezi
shirikishi.”amesema Mworia
Mworia amesema tovuti hiyo imeanza mwaka 2017 na tayari wamewafikia
jumla ya wanafunzi wapatao 150,000.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo