Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza
Hadi kufikia Machi 31,2025, vivuko vinne kati ya vitano vitakavyofanya kazi ndani ya Ziwa Victoria,vinatarajia kukamilika na kusaidia wananchi wa Wilaya za Magu, Ukerewe, Bunda,Misungwi na Sengerema.
Hayo yamebainishwa Januari 24,2025,wakati wa ziara ya ,Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega,ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa vivuko hivyo, unaotekelezwa na Mkadarasi mzawa kampuni ya Songoro Marine Transport,katika karakana ya kampuni hiyo iliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Ulega amesema,Serikali kupitia Wakala wa Ufundi Tanzania(TEMESA), imefanya uwekezaji wa bilioni 56,kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vivuko katika maeneo mbalimbali.
Ambapo kati ya fedha hizo bilioni 33 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa vivuko vipya 6, kati ya hivyo vitano vitatoa huduma ndani ya Ziwa Victoria ambavyo ni Kisorya-Rugenzi(Ukerewe-Bunda),Ijinga-Kahangala(Magu),Bwiro-Bukondo(Ukerewe).
Vingine ni Nyakaliro-Kome(Sengerema) na Buyangu-Mbalika(Sengerema-Misungwi) huku kimoja kitafanya kazi Bahari ya Hindi eneo la Nyamisati-Mafia(Mkulanga-Mafia.
“Nikuagize Mkurugenzi Mkuu wa TEMESA,katika uwekezaji huu ufanye tathimini ya kiuchumi na kijamii,ambayo wananchi wa maeneo haya wataipata kutokana na vivuko hivi,”amesema Ulega.
Pia amesema,bilioni 23, zimewekezwa na Serikali katika kufanya ukarabati wa vivuko saba,kikiwemo cha Mv.Nyerere,Mv.Kilombero II,Mv.Magongoni,Mv.Ukara,Mv.Ruhuhu,Mv.Old Ruvuvu na Mv.Kigamboni.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji Mkurungezi wa kampuni ya Songoro Marine Transport,Major Songoro,amesema,hadi kufikia Machhi 31,2025,vivuko vine kati ya vitano vitakuwa vimekamilika huku kimoja kikitarajiwa kukamilika Julai 4,2025.
Songoro amesema,Kivuko cha Bwiro-Bukondo utekelezaji wake umefikia asilimia 90.7,kitakamilika Machi 31,2025,Rugenzi-Kisorya kimefikia asilimia 84.5 kinatarajia kukamilika Machi 29,2025, Nyakarilo-Kome utekelezaji ni asilimia 83.19,Ijinga-Kahangala asilimia 90.7,na kitakamilika Machi 31,2025 huku kivuko cha Buyangu-Mbalika kimefikia asilimia 80.5,na kinatarajia kukamilika Julai 4,2025.
Kwa upande wake Mbunge wa Sengerema,Hamiss Tabasamu,amesema, wao vivuko ni maisha kwa sababu ya Ziwa Victoria,ambapo wananchi walikuwa wanapata tabu hivyo amepongeza Serikali kwa uwekezaji huo wa vivuko vipya vitano,ambavyo siyo kuwa vimemaliza changamoto ya wananchi ila angalau kutakuwa na unafuu.
“Leo wananchi wa Buyangu wakipata kivuko hicho cha Buyangu-Mbalika,tutawanusuru na vifo wananchi takribani 30 kila mwaka,ambao wanavuka na mitumbwi kutoka upande wa Sengerema kwenda Misungwi,”.
More Stories
Mashirikisho yaunga mkono azimio mkutano mkuu CCM
Watumishi wa Mahakama waonywa
CCM ilivyotambua mchango wa wanahabari Mkutano Mkuu Maalum