Na Mwandishi wetu,Timesmajira
WAKALA wa vipimo mkoa wa kinondoni (WMA) wametoa rai kwa wananchi kuendelea kutumia vipimo sahihi vya Pekee katika kumlinda mlaji kwa kupata bidhaa bora zenye viwango kwa matumizi halali.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam, meneja wa Wakala hao mkoa wa kinondoni Lilian Mombheki amesema kuwa kumekuwa na hulka kutoka kwa baadhi ya watu kuendelea kutumia vipimo visivyo halali kwa makusudi Ili kujinufaisha wao.
“Suala la kutumia mzani kwa walaji ni muhimu ambapo nchi mbalimbali wamebaini kwamba matumizi ya vipimo hualalisha usawa wa bidhaa kwa mnunuzi na muuzaji ,”amesema Mombheki .
Aidha meneja wa Wakala hao amesema kwamba kwa mwaka huendesha zoezi la uhakiki wa mizani pamoja na utoaji wa elimu katika kutumia vipimo sahihi kwa bidhaa salama kwa watumiaji.

Kilele cha siku ya vipimo duniani hufanyika mei 20 ya kila mwaka kauli mbiu ya mwaka huu inaongozwa na ujumbe usemao vipimo hujenga Imani katika sera za biashara na uchumi ambapo kila mfanyabiashara lazima awe na Imani na Soko lake katika kumlinda mteja dhidi ya upatikanaji wa bidhaa salama na usahihi wa vipimo.
Hata hivyo Wakala hao amesema uwachukulia hatua za kisheria kwa kuwatoza faini wale wote wanaokiuka utaratibu wa kuuza ama kununua bidhaa zisizo na ubora kwa lengo la kuwauzia wengine.

More Stories
Timu 20 kushiriki Mwijage Cup
Mixx yajivunia ongezeko la Wateja kupitia kampeni yake
Airtel,Serikali waungana kupanda miti Bagamoyo na kusafisha fukwe Dar