November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wakuu China, Poland na Cuba kutembelea Tanzania

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Diplomasia ya Tanzania yazidi kuimarika huku fursa mbalimbali za kimaendeleo zitokana na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi mbalimbali ulimwenguni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea ugeni mkubwa wa viongozi kutoka nchi tatu kwa mwezi huu wa Januari pamoja na Februari lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Hapo kesho Januari 22, 2024, Rais Samia anatarajia kumpokea Mheshimiwa Liu Guozhong Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China anayekuja nchini kwa ziara ya siku tatu.

Katikati ya ujio wa kiongozi huyo wa China, tarehe 23 ya mwezi huu rais Samia atapata ugeni mwingine wa Makamu wa Rais wa Cuba, Mheshimiwa Salvador Valdes Mesa atakayekaa nchini kwa siku tatu lengo likiwa ni kukuza mahusiano ya nchi hizi mbili. Baadhi ya mambo atakayofanya Mhe. Valdes ni na viongozi wengine wakubwa wa nchi, Bara na Zanzibar, kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa ya Biolarvicide cha Kibaha na kusalimiana wa Watanzania waliosoma Cuba.

Rais wa Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda anatarajia kuwa na ziara ya kikazi tarehe 8 na 9, Februari, 2024 katika hatua ya kuimarisha diplomasia ya Tanzanua na Poland ambao wana uhusiano mzuri katika miradi ya maendeleo ya miundombinu, uhifadhi wa wanyama pori, elimu, maji na usimamizi wa mazingira, utalii, biashara na uwekezaji bila kusahau ushirikiano wa mabunge.

Mbali na viongozi hawa kuja Tanzania, Rais Samia amealikwa kufanya ziara za Kitaifa Indonesia, Vatican na Norway. Hii ni ishara kuwa Tanzania inazidi kufungua mipaka yake kimataifa na kuwa ina ushirikiano mzuri wa kidiplomasia na mataifa mengine.