January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa Kimila Tarafa za Loliondo na Ngorongoro wawasilisha ripoti maalum

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Viongozi wa kimila kutoka katika tarafa za loliondo na ngorongoro wamefanikiwa kuwasilisha ripoti maalumu ya mapendekezo ya maoni ya wananchi

Kamati hiyo imewasilisha taarifa hiyo hivi karibuni kwa waziri mkuu Kasimu Majaliwa

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Kiongozi wa kimila (Lagwanani) Bw Metui ole shaudo Alisema kuwa Ripoti hiyo imebeba mapendekezo na maoni ya wananchi wa tarafa hizo

Alidai kuwa moja ya maendekezo ambayo ipo katika Ripoti hiyo ni uwepo wa Ngorongoro ambayo wanaitaka na sio ile ambayo wataalamu wanaitaka

“Tumeweka Ripoti kwa kukusanya maoni ya wananchi wote na mapendekezo ambayo tunaitaka sanjari na uhalisia”alisema

Naye mjumbe wa kamati hiyo Bi Mageth Kaisori alisema kuwa hapo awali kulikiwa na taarifa za ongezeko la watu na mifugo

Kaisori alisema kuwa kuna taarifa ambazo zinasemwa mtaani lakini sio kweli kabisa

“Kwa mfano inasemekana Ngorongoro hakuna tena msitu wakati mpaka asubui ya Leo nimepigiwa simu kuwa tembo wamezuia watoto,nataka kusema kuwa hata hao tembo wameongezeka “aliongeza Kaisori

Wakati mwenyekiti wa baraza la wafugaji bw Edward Maura Alisema kuwa wao wanamuomba sana Raisi Samia Suluhu Aweze kuangalia Ripoti hiyo lakini hata kuifanyia kazi kwa wepesi

Alidai kuwa kwa kipindi hiki cha kuelekea kiangazi huwa wanateswa sana na wahahifadhi hali ambayo inasababisha hata mifugo yao kufa