November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa dini wana nafasi kubwa kukemea jamii kuepuka ukatili wa kijinsia dhidi ya wakemvu -Naibu Waziri Afya Ofisi ya waziri mkuu Ummy

Na David John

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera Bunge Kazi Ajira Vijana na watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya juu ya kuelimisha jamii kuepuka vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu .

Amesema kuwa kuna haja ya viongozi hao kuendelea kusaidia kwenye eneo hilo kwa maana kuelimisha huku akiitaka jamii hiyo yenye ulemavu kujitokeza hadharani na kujiona kama wanaweza na kamwe asione aibu badala yake ajione kuwa anaweza.

Naibu waziri Ummy ameyasema haya leo jijini Dar es Salaam katika katika Ufunguzi wa kongamano la kitaifa kuhusu jinsi gani Wanawake na Vijana wenye ulemavu wanaweza kufikia Haki zao za kuishi maisha Huru dhidi ya ukatili Tanzania.

Amesema kuwa ipo haja ya kushirikiana kwa pamoja na kuwajengea uwezo wanawake hususani wakemavu ili nawenyewe waweze kusisima na kujiamini nakwamba wakijengewa uwezo baadae wanajiamini .

“Nataka niwaleze kuwa juhudi zote zinazofanywa hususani kwa watu wenye ulemavu lengo ni kupata haki yao ya msingi na wakifanya hivyo watapiga hatua lakini kikubwa nikutokata tamaa” amesema

Katika hatua nyingine Naibu waziri Ummy amewahamasisha walemavu kujitokeza Mahospitali na vituo vya afya kupima afya zao nakwamba katika hilo wasione aibu .

Pia ameongeza kuwa katika mwaka ujao Taifa linakwenda kufanya sensa ya kuhesabiwa ili kujua au kupata takwimu halisi hivyo mchakato utakapofika wajitokeze.

Kuhusu ukatili amefafanua kuwa tatizo hilo nikubwa na kila mmoja anapaswa kuendelea kupinga na kukemea huku akitoa raia kwa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo Barani Afrika WiLDAF kufanya tathimini juu ya ukubwa wa tatizo hilo na ofisi ya waziri mkuu iko wazi kupokea yale ambayo wataafikiana.

“Kwa ujumla na wahimiza kwamba msikate tamaa kwani nyie mnaweza na kama kuna watu watawakatisha tamaa semeni ofisi ya waziri mkuu.imesema tunaweza .kikubwa ni upendo na ushirikiano.”amesisitiza

Pia uzinduzi wa kongamano hilo ulienda sambamba na uzinduzi wa mpango wa mradi wa My Choice my right ambao ni wama ambao unatafasili ya kulinda haki za wanawake na wasichana wenye ulemavu Tanzania.

Kwaupande wake Anna kulaya wakili ,mratibu kitaifa kutoka shirika la wanawake katika sheria na maendeleo Barani Afrika WiLDAF amesema kuna haja na umuhimu wa kuwepo madawati ya kijinsia yanayowalenga watu wenye ulemavu .

” leo tunajadili mambo mengi ,Sera ,mifumo kwa ajili ya watu wenye ulemavu kumsingi tunahitaji kujadili mambo mengi na tunashukuru wadau wote kwa kujitoa kwao kwetu na kongamano hili litaibua fursa ya kuangalia mambo mengi yanayohusu walemavu.”amesema

Naye Askofu Dkt Fredrick Shoo ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la kikristo Tanzania( CCT)na mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT akizungumza katika ufunguzi wa kongamano amesema viongozi wa dini wanatambua watu wote bila kuwepo kwa ubaguzi na kuheshimu haki ya kila mtu japo kuna wengine wanafanya ukatili.

Ameongeza kuwa watu ambao wanashiriki katika kufanya vitendo hivyo waache ,wabadilike na watubu kwani maandiko kupitia vitabu vyote yanapinga vitendo hivyo hivyo viongozi wa dini wasimame pamoja na kuungana na wote wanaotetea haki za walemavu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu .Sera Bunge, Kazi, Ajira ,Vijana na watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga (katikati) mwenye magongo akiwa akiwa katika picha na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia kwenye ufunguzi wa kongamano la kitaifa kuhusu namna gani wanawake na vijana wenye ulemavu wanaweza kufikia Haki zao za kuishi maisha yaliyo Huru Dhidi ya ukatili Tanzania.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu .Sera Bunge, Kazi, Ajira ,Vijana na watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la kupinga vitendo vya ukatili dhidi walemavu jana jijini Dar es Salaam