Na Esther Macha, Timesmajira,Online,Mbeya
SERIKALI imewaonya viongozi wa Dini wanaowakataza waumini wao kutumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa madai kuwa ugonjwa huo unaponywa kwa maombi pekee yake.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya , Dkt.Vicent Anney wakati wa wa Kongamano la kitaifa la Vijana na Viongozi lenye lengo la kujadili changamoto zinazowakabili vijana kuhusu Virusi vya Ukimwi linalofanyika jijini Mbeya.
“Ndugu zangu viongozi wa dini naombeni tuwe mfano kuwasaidia waumini wenu wanywe dawa na sio kukataza ,nyie muwe mstari wa mbele kuisaidia serikali “amesema Dkt.Anney.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa baadhi ya viongozi wa dini hawatoi tahadhari kwa vijana wanaoishi na vvu na ukimwi kwa kuamini kwamba maombi pekee na imani inaweza kusaidia uponyaji.
“Lakini kuna dhana pia ya kufuata mila na desturi ambazo zinaweza kusababisha kuwepo kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi hasa kundi la vijana na wanaume”amesema mkuu huyo wa wilaya.
Mwakilishi wa Jumuiya ya kikristo Tanzania (CCT) Dkt. Basilisa Ndonde amesema kweli kuna baadhi ya viongozi wa dini walisema changamoto hiyo ipo na kwamba elimu zaidi inahitajika ili viongozi hao kuwa mabalozi wazuri kuhimiza waumini kutumia dawa za kufubaza makali ya Ugonjwa wa Ukimwi.
“Ni kweli hii changamoto ipo kukosa elimu kwa baadhi yetu hivyo tunahitaji elimu zaidi katika kuwasaidia waumini wetu na viongozi wa dini ili elimu hii iweze kusaidia kulinda vizazi vyetu”amesema.
Beatrice Mutayobba ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto amesema Wataalam wa Sekta ya Afya nchini wamekutana jijini Mbeya kufanya Mkutano wa mwaka wa kwa waganga wakuu wa Mikoa, Wilaya na waratibu Ukimwi kujadili mpango wa Taifa wa kudhibiti ukimwi wa miaka mitano kuanzia 2020-2025.
More Stories
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba
Ng’ombe 10 wamekufa kwa kupigwa na radi
Rukwa waanzisha utalii wa nyuki