Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Simiyu
SHEKHE Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu Mahamud Kalokola amesema Hayati Rais John Magufuli alifanya mengi hasa kwa Watu wanyonge ambao kwa kiasi kikubwa alikuwa akiwatetea.
“Hayati Rais Magufuli amefanya Mambo makubwa, alikuwa mtetezi wa wanyonge. Kikubwa tumuombe huko aliko mungu ampunguzie adhabu ya kaburi” amesema Shehe Kalokola.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga amesema Hayati Rais Magufuli alijipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge na kwamba ni vema Watanzania wakaendelea kunuenzi na kumkumbuka kwa mema aliyoyafanya.
Ibada hiyo maalum ilifanyika katika Viwanja vya CCM Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu Na kwamba iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Viongozi wa dini wakiwemo wa Kanisa Katoriki, KKKT, Kanisa la Halisi la Mungu Baba, Kanisa la Wasabato.
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani