December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa Chadema kumpokea Lissu uwanja wa ndege leo mchana

Na Penina Malundo, TimesMajira Online, DSM

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameondoka Ofisi za Makao Makuu wamewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara) . Tundu Lissu .

Lissu atatua uwanjani hapo saa 7.20 mchana huu. Baada ya kupokelewa JNIA, Makamu Mwenyekiti huyo ataelekea Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam, ambako atazungumza na Waandishi wa Habari.