Na Mwandishi wetu,timesmajira,online
KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo,Ado Shaibu,amekabidhi kadi za uanachama kwa uongozi wote wa Chama cha Wananchi CUF wa kata ya Tinginya na vijiji vyake vya Tinginya, Tanga na Namatanda jimbo la Tunduru Kaskazini.
Viongozi hao waliopewa kadi za ACT-Wazalendo wakiongozwa na Mwenyekiti wa kata, Mshamu Baniani, ni pamoja na Katibu aliyekuwa chama hicho cha CUF , Salumu Bomba na aliyekuwa Mgombea udiwani kupitia tiketi ya chama hicho Mohamed Ndayani na wanachama wengine.
“Jana nilipata wito wa viongozi wa CUF wa Kata ya Tinginya walionitaka nirudi kwa ajili ya mazungumzo,walisema wameguswa na kitendo changu cha kupita kushukuru ,Viongozi hawa wa Kata, kama ilivyokuwa kwa viongozi na wanachama wengi wa CUF Tunduru, kinyume na maelekezo ya Chama chao, waliniunga mkono nilipogombea Ubunge katika Jimbo la Tunduru Kaskazini walitanguliza mbele maslahi ya Tunduru na mageuzi kuliko ya Chama chao,”amesema na kuongeza
‘Jana waliponiita walisema bayana kuwa kitendo changu cha kuja kushukuru kimewatia moyo sana na wameona ACT Wazalendo ni jahazi sahihi hivyo wameona bora wajiunge kwetu,” amesema
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â