Na Rose Itono,Timesmajira
Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazotolewa kwa wazawa kwa kuwa Wabunifu na wavumbuzi
wa miradi ambayo itaweza kuleta utatuzi wa changanoto
zilizopo nchini na duniani kote
Akizungumzai kwenye mkutano wa mwaka wa Vijana na Sayansi na Teknolojia 2025 ulioandaliwa na Taasisi inayoshughulika masuala ya vijana katika Sayansi na Teknolojia ya Seris Foundation Dar es Salaam Leo Meneja
Kitengo Cha Utatuzi wa Changamoto za Uwekezaji kutoka Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Latifa Kigoda amesema Kituo Cha Uwekezaji Tanzania kina jukumu la kuwaandaa vijana kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ili waweze kuwa wafanyabiashara na wawekezaji wa baadaye
Amesema kutokana na hali hiyo
Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC ) kina jukumu la kunadi fursa za Uwekezaji kwa wazawa, wageni na vijana hivyo vijana wana kila sababu ya kukumbushwa namna gani wanaweza kuwa wawekezaji wa baadaye kwa kutambua kuwa elimu tayari wameshaipata kwenye masuala ya Sayansi na Teknolojia
“Kutokana na hatua hiyo vijana mnapaswa kuwa wabunifu na wavumbuzi wa miradi ambayo itaweza kuleta utatuzi wa changanoto
zilizopo nchini na duniani kote,” amesema Kigoda
Amesema ulimwengu wote sasa unaelekea katika masuala ya Sayansi na Teknolojia kwa hivyo kutokana na hali hiyo watanzania hatupaswi kubaki nyuma
“Tumejionea wazi namna SerikaliI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inavyoweka mazingira mazuri ya kuendeleza Tasnia ya Sayansi na Teknolojia na pia kwenye biashara na Uwekezaji hivyo tunapaswa kuunga mkono hatua hiyo kwa kuhakikisha fursa zote zinazopatikana tunazitumia ipasavyo,” ameongeza Kigoda
Aidha ameipongeza Taasisi inayoshughulika na vijana katika masuala ya Sayansi na Teknolojia ya Seris Foundation ambayo imeanzishwa mwezi Mei 25 2024 kwa kuwezesha vijana zaidi ya 100 kugundua na kukuza vipaj
Pia amewapongeza kwa kuandaa mkutano huu ambao utawawezesha
vijana wasomi wa taaluma ya Uhandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kutimiza ndoto zao za kujiletea maendeleo
Kwa upande wake Mkurugenz Mtendaji wa Taasisi ya Seris Foundation ambao ndiyo waandaaji wa mkutano huo
CPA Debora Wami ameipongeza Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ( AQRB) na Bodi ya Wahandisi (ERB) kwa kuwaunga mkono kwa kufadhili mkutano huo ambao umeweza kuwakutanisha vijana zaidi ya 200
“Ndani ya kipindi cha mwaka tangu Taasisi hii ianzishwe imeweza kujipambanua
kama jukwaa madhubuti la kukuza vipaji, kujenga ujuzi, na kuhamasisha ujasiriamali kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” amesema CPA Wami
Amesema vijana wa Kitanzania, hasa katika sayansi, teknolojia, wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi wameweza kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi yao.
More Stories
Sheikh Ponda kutua rasmi Act Wazalendo
Puma Energy Yazindua Mradi wa Umeme wa Jua kwa Kiwanda cha Alliance One
Taasisi ya Jalaram Seva Mandal yatoa msaada kwa Watanzania