Na Penina Malundo, Timesmajira Online
KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) Wilayani Kilosa, Philbert Kipenda amewataka Makundi ya Vijana chini ya miaka 35 wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za Ubunge wa Jimbo la Kilosa, Mikumi, Ubunge wa Viti Maalum kupitia UVCCM na UWT, Udiwani wa Kata na Udiwani wa Viti Maalum.
Kipenda ameuambia mtandao wa Timesmajira kuwa, fomu zitaanza kutolewa Julai 14 hadi 17 mwaka huu kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.
“Kwa fomu za Ubunge zitatolewa Ofisi ya Katibu wa CCM Wilaya na fomu za Udiwani zitatolewa Ofisi ya Katibu wa CCM Kata huku fomu za Viti Maalum Ubunge kupitia UVCCM zitatolewa Ofisi ya Katibu wa UVCCM Mkoa, Ubunge Viti Maalum kupitia UWT zitatolewa Ofisi ya UWT Mkoa na Udiwani wa Viti Maalum fomu zitatolewa Ofisi ya Katibu wa UWT Wilaya,” amesema Katibu huyo.
Amesema, wao kama viongozi wa UVCCM ngazi ya Kata na Matawi wanao wajibu wa kuhamasisha wanachama kupitia makundi mbalimbali ya vijana kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za uongozi 2020/2025.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote